" ZOEZI LA UCHUKUAJI NA UREJESHAJI FOMU 2025 LAFANYIKA KWA TIJA , WANAWAKE WAITIKIA KWA WINGI SHINYANGA

ZOEZI LA UCHUKUAJI NA UREJESHAJI FOMU 2025 LAFANYIKA KWA TIJA , WANAWAKE WAITIKIA KWA WINGI SHINYANGA

 


Zoezi la kuchukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi za udiwani na ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) limehitimishwa kwa mafanikio makubwa katika Wilaya ya Shinyanga Mjini, huku wanachama wa chama hicho wakijitokeza kwa wingi kushiriki hatua hiyo muhimu ya kidemokrasia.

Katika ngazi ya ubunge, hadi zoezi linapofungwa Jumatano, Julai 2, 2025, watu zaidi ya wanane walikuwa wamechukua fomu kuwania Jimbo la Shinyanga Mjini. Baadhi yao ni:

·         James Jumbe Wiswa

·         Eunice Jackson Wiswa

·         Paschal Patrobas Katambi

·         Stephen Julius Masele

·         Gilitu Nila Makula

·         Paul Joseph Bulandi

·         Vumilia Mtaki Amos

·         Elvis Benedict Lyaruu

Zoezi hilo pia limehusisha mwitikio mkubwa wa wanawake katika nafasi za uongozi, ambapo hadi kufikia mwisho wa mchakato wanawake zaidi ya 14 walichukua fomu za kuwania ubunge wa viti maalum Mkoa wa Shinyanga. Baadhi yao ni:

1.    Salome Makamba

2.    Mwanahamis Athuman

3.    Zawadi Dickson

4.    Christina Gulle

5.    Felister Buzuka

6.    Quine Elizabeth Makune

7.    Florah Kishiwa

8.    Jovina Mlindwa

9.    Janeth Seni

10.  Florah Parangyo

11.  Christina Mnzava

12.  Asella Magaka

13.  Santiel Kirumba

14.   Harris Kyanila

Katika majimbo baadhi ya wania nia: Katika Jimbo la Solwa, waliowasilisha nia ya kugombea ni pamoja na Keflen Henry Maganga na Angelina Maganga lakini pia Jimbo la Ushetu ni pamoja na Emmanuel Cherehan, Aidha Jimbo la Itwangi ni pamoja na Richard Raphael Maselejimbo la Msalala ni pamoja na Ezekiel Maige huku jimbo la Kahama mjini ni pamoja na Salum Ismail.

Kwa upande wa udiwani, Baadhi ya watia nia kutoka kata mbalimbali pia walijitokeza kwa kasi, akiwemo Victor MkwizuMwajuma K. Mbogo, mwanamke mwenye ulemavu aliyevutiwa na hotuba za Rais Samia Suluhu Hassan, Mwalimu James Msimbang’ombe, Hatibu Mgeja, Alfred Alex NyasaniFlavian Makwaiya pamoja na Jackline Isaro naye ameonesha nia ya kuwania nafasi ya udiwani kata hiyo ya Ngokolo, Peter Alex Frank (Mr. Black) wa Kizumbi, Mwalimu Naomi Kache, Ganai Hassani wa Chamaguha na Abdallah Maulid Abdallah wa Masekelo.

Katika Kata ya Ngokolo, zoezi hilo limeelezwa kufanyika kwa tija na amani, likihusisha makundi yote ya kijamii wakiwemo vijana, wanawake na wazee. Katibu wa CCM kata hiyo, Kichele Werema, amesema mwamko ulioonekana ni ishara ya mapenzi ya dhati kwa chama, na kwamba taratibu zote zilizowekwa zimezingatiwa kikamilifu.

Amesema anaamini mwitikio huo utaleta ushindani wa kistaarabu utakaochochea maendeleo endelevu kwa wananchi wa Ngokolo, akibainisha kuwa nidhamu na ushirikiano wa wanachama ndiyo silaha ya ushindi wa kweli.

Zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu lilianza rasmi Jumamosi, Juni 28, 2025, na likahitimishwa Jumatano, Julai 2, 2025, kwa mujibu wa ratiba ya Chama Cha Mapinduzi.

WATIA NIA UBUNGE – SHINYANGA MJINI (Bofya Majina)

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post