Na Mapuli Kitina Misalaba
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Keflen Henry Maganga, amejitokeza kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Solwa kwa kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo kupitia CCM.
Tukio hilo limefanyika leo Jumanne Julai 1, 2025, katika ofisi za CCM Wilaya ya Shinyanga vijijini, ambapo Maganga.
Akizungumza baada ya kuchukua fomu hiyo, Keflen Maganga amesema amejipanga kuiwakilisha vyema Solwa endapo atapewa ridhaa na chama chake, huku akisisitiza kuwa anayo nia ya dhati ya kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo kwa kushirikiana nao katika kupanga vipaumbele vyao.
Uchukuaji wa fomu unaendelea kwa wanachama mbalimbali wa CCM wanaowania nafasi za udiwani na ubunge kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Post a Comment