" MFUMO WA KIDIGITALI KUWATAMBUA NA KUWAHUDUMIA WATU WENYE ULEMAVU

MFUMO WA KIDIGITALI KUWATAMBUA NA KUWAHUDUMIA WATU WENYE ULEMAVU

Na Lucas Raphael,Tabora

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Zuhura Yunus, amewataka  Maafisa TEHAMA na Maafisa Ustawi wa Jamii kuhakikisha wanatumia mfumo wa kielektroniki wa kuwatambua watu wenye ulemavu nchini (PD-MIS).

Kauli hiyo ilitolewa jana wakati akizungumza  wa ufunguzi, wa mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Hoteli ya JM, mkoani Tabora .
 
Zuhura alisema kwamba mafaunzo hayo yenye lengo la kuwajengea uwezo watendaji hao kuhusu matumizi ya mfumo wa PD-MIS, ili wanaporejea katika maeneo yao ya kazi waanze mara moja kusajili na kuwaunganisha watu wenye ulemavu na huduma mbalimbali zinazotolewa na Serikali.

Alibainisha kwamba  mfumo huo utawezesha Serikali kupata takwimu sahihi na kwa  wakati kuhusu watu wenye ulemavu, hivyo kurahisisha utoaji wa huduma stahiki kama vile usajili rasmi, upatikanaji wa vifaa saidizi, mikopo isiyo na riba ya asilimia 2, na fursa za ununuzi wa umma kwa makundi maalum.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kitengo cha Watu wenye Ulemavu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Rasheed Maftah, alibainisha kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa kitaifa, yakiwa ni ya awamu ya tatu baada ya kufanyika kwa mafanikio katika kanda ya ziwa na kanda ya kati.

Kwa hatua hii, Tanzania imeandika historia ya kuwa nchi ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki kuanzisha na kutumia mfumo wa kidijitali kwa ajili ya utambuzi na ufuatiliaji wa huduma kwa watu wenye ulemavu, ikiwa ni sehemu ya dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita kuhakikisha hakuna mwananchi anayeachwa nyuma katika maendeleo.
Mafunzo hayo maalum ya siku tatu kwa Maafisa TEHAMA na Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka mikoa ya Tabora, Kigoma na Katavi
Mwisho

 

Post a Comment

Previous Post Next Post