
TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewataka Waratibu wa Uchaguzi wa Mikoa ,Wasimamizi wa Uchaguzi,Wasimamizi wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maofisa uchaguzi na maofisa ununuzi kutenga sehemu ya muda wao kusoma Katiba, sheria na maelekezo yanayotolewa na Tume hiyo.
Kauli hiyo ilitolewa na mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Magdalena Rwebangira,wakati amehitimisha rasmi mafunzo ya siku tatu kwa washirikia kutoka mikoa ya Tabora na Kigoma yalitofanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha saut mkoani hapa.
Alisema kwamba lengo la kusoma Katiba,sheria kanuni na miongozo na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Tume hiyo ili kuweza kusimamia vyema uchaguzi utakaokuwa huru na haki.
Rwebangira liendelea kueleza kwamba shughuli zote za uchaguzi zinaongozwa na Katiba , sheria , kanuni , maadili ya uchaguzi na maelekezo ya Tume hivyo mkikutana na changamoto zozote msisite kufanya mawasilino na watendaji wa Tume
Hata hivyo aliwataka waratibu na wasimamizi wa uchaguzi wa ngazi ya jimbo, kuyatumia maaarifa waliyoyapata kwa weledi mkubwa ili kuhakikisha uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani unafanyika kwa ufanisi mkubwa na kwa kuzingatia sheria za nchi.
Aidha Rwebangira aliwataka wasimamizi kuhakikisha wanawafundisha watumishi wa tume walio chini yao kwa umakini na uadilifu, huku wakizingatia sheria, kanuni na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
sanjali na hilo aliwakumbusha umuhimu wa kuwasiliana na wananchi kwa uwazi kupitia vyombo vya habari, lakini akasisitiza kuwa taarifa zozote zinazotolewa lazima wajirishishe kwanza na zihakikiwe kabla ya kutangazwa ili kuepusha taharuki kwa wananchi.
“Usikurupuke kutoa taarifa, ni vyema ukashirikiana na wenzako kabla ya kuzungumza hadharani,” alisema kwamba Rwebangira .
aliendelea kutoa ufafanuzi kuwa mara baada ya kula kiapo, kila mmoja wao ni mtumishi wa Tume na anapaswa kutunza siri za kazi kwa mujibu wa Kanuni ya 8 ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2025.
Alionya kuwa kuvujisha taarifa za ndani ni kuvunja sheria na kiapo cha uaminifu.
Katika mafunzo hayo, washiriki walifundishwa kuhusu mabadiliko ya sheria za uchaguzi, taratibu za upigaji kura, usimamizi wa maombi ya kupiga kura nje ya vituo, pamoja na namna ya kutoa taarifa za mapungufu au kasoro za vifaa vya uchaguzi pindi vinapopokelewa.
Mafunzo yalijumuisha pia maandalizi ya kutoa elimu kwa wasimamizi wa kata na watendaji wa vituo vya kupigia kura.
Kupitia mafunzo hayo, Tume inalenga kuhakikisha kuwa uchaguzi wa mwaka 2025 unafanyika kwa njia ya uwazi, ufanisi na kuzingatia misingi ya demokrasia, kwa manufaa ya taifa na wananchi wote.
Mwisho


Post a Comment