" MKANDA WA SURUALI WAGEUKA KUWA KITANZI

MKANDA WA SURUALI WAGEUKA KUWA KITANZI



Na: Belnardo Costantine, Misalaba Media.

Mtu mmoja mwenye jinsia ya kiume aliyetambulika kwa jina la  Omari Said Bakari  (35),  mkaazi wa Kijiji cha madanga  mkoani lindi  amekutwa amefariki dunia kwa kujinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali.

Inaelezwa kuwa  alitumia mkanda kujinyonga kwa kuufunga 
  kwenye tawi la Mti wa Mkorosho kisha kujitundika hadi umauti ulipomkuta.

Tukio hilo lilitokea Julai 22, 2025 majira ya saa tatu asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi mkoa wa Lindi, tukio hilo limethibitishwa na uchunguzi wa awali umeonesha kuwa Marehemu alikuwa akipitia hali ya msongo wa mawazo kwa muda mrefu. Ndugu wa karibu pamoja na majirani waliokuwa wakiishi naye wameeleza kuwa hali hiyo huenda ndiyo iliyomsukuma kuchukua uamuzi huo mgumu.

Jeshi la Polisi limeeleza kuwa hakuna dalili za tukio hilo kuhusishwa na vitendo vya uhalifu na kwamba uchunguzi zaidi unaendelea ili kubaini kwa undani sababu za kisaikolojia au kijamii zilizochangia hatua hiyo. Aidha, limesisitiza umuhimu wa jamii kuimarisha usaidizi wa kisaikolojia kwa watu wanaoonesha dalili za msongo wa mawazo au matatizo ya kiakili.

Mwili wa marehemu tayari umekabidhiwa kwa familia yake kwa ajili ya taratibu za mazishi. 

Post a Comment

Previous Post Next Post