" MKOA WA KAGERA UTAJWE KAMA KANDA MAALUM KUKABILIANA NA MAAFA

MKOA WA KAGERA UTAJWE KAMA KANDA MAALUM KUKABILIANA NA MAAFA


Na mwandishi wetu, Misalaba Media 
Bukoba

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mh. Erasto Sima ameiomba Serikali kuutambua Mkoa wa Kagera kama kanda maalum katika kukabiliana na maafa kutokana na majanga yanaoukumba mkoa huo mara kwa mara.

Amezungumza hayo wakati akifunga mafunzo ya siku mbili ya kamati elekezi na kamati ya wataalam ya maafa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba yaliyofanyika katika makao makuu ya Hamshauri ya Wilaya ya Bukoba tarehe 21 na 22,Julai 2025.

Sima ameeleza mkoa21 na 22,Julai 2025.
 my Sima ameeleza mkoa wa wa KAGERA umekua ukikumbwa na maafa ya mara kwa mara ikiwemo tetemeko la ardhi,mvua za upepo,radi na magonjwa ya mlipuko kama maburg na kipindupindu.

Kufuatia hali hiyo  ameeleza ghala la sasa la kukabiliana na maafa lipo mkoani Shinyanga hivyo panapotekea tatizo inachukua muda mrefu kusafirisha vifaa vya uokozi pamoja na mahitaji mbalimbali kwa waathirika, Hivyo kupelekea kuiomba Serikali iangalie namna ya kuufanya mkoa wa Kagera kuwa kanda maalum kwa kuipatia ghala la kupambana na maafa pamoja na wataalam.

"Tumekua tukiwajibika hasa katika Halmashauri zetu kuweka bajeti za kuweka mitego ya radi katika taasisi zetu zikiwemo ofisi,shule,zahanati na vituo vya afya" aliongeza Sima.

Katika hatua hiyo katibu tawala wa Wilaya ya Bukoba Bi Proscovia Jaka Mwambi alitoa wito kwa kamati zote kuyafanyia kazi kwa vitendo mafunzo haya ili kuepukana na majanga yanayoepukika badala ya kusubiri wakati wa maafa ndipo kamati zifanye kazi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Bi. Fatina Hussein Laay, aliwashukuru wawezeshaji kutoka ofisi ya waziri mkuu kwa kushirikiana na shirika la World Vision Tanzania kwa kuendesha mafunzo haya na kuahidi kamati ya wataalam kutoka ofisi yake itayafanyia kazi yale yote waliyojifunza.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post