
Edwin Soko (TMFD)
Tanga
Mkurugenzi wa Uvuvi toka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Mohammed Sheikh amewasilisha vipaumbele vinne vya Wizara kwenye sekta ya uvuvi Kwa Mwaka 2025 - 2025 mbele ya mashirika ya yasiyo ya kiserikali leo Jijini Tanga.
Prof.Sheikh amevitaja vipaumbele hivyo kuwa ni, kuongeza uzalishaji na kupata masoko na kuongeza thamani ya mazo ya uvuvi, kuimarisha ulinzi na usimamizi wa rasilimari za uvuvi, kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya uvuvi na kuimarisha utafiti, na mafunzo kwenye sekta ya uvuvi.
" Hivyo kama Kuna mashirika yoyote yanayoweza kuunga mkono jitihada zetu hizi kwenye vipaumbele nilivyovitaja basi nawakaribisha ili tufanye kazi kwa pamoja Kwa kuwa sekta ya uvuvi ni yetu na lazima tuipende" Alisema Prof. sheikh.
Naye Bwana Tumaini Chambua, Mratibu wa dawati la NGO toka Wizara ya mifugo na uvuvi alisema kuwa, kikao hicho kinatoa nafasi ya kukaa kwa pamoja na kujadiliana juu ya sekta ya uvuvi na kuweka mipango mathubuti ya namna ya kuimarisha mashirikiano baina na Wizara ya mifugo na uvuvi na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Pia chambua alipata nafasi ya kuwasilisha mwongozo wa mashirikiano baina ya Wizara na Asasi za kiraia na Wizara.
Kikao hicho ni Cha siku mbili Julai 21 na 23 , 2025 na kinafanyika kwenye hotel ya Nyinda Classic Jijini Tanga.
Post a Comment