Na Mapuli Kitina Misalaba
Afisa Ununuzi na Ugavi wa Wakala wa
Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Shinyanga, Alfred Alex Nyasani, maarufu kama Nyasani, leo Julai 2, 2025, ameonyesha dhamira ya kuwatumikia
wananchi kwa sura mpya baada ya kuchukua
na kurejesha fomu ya kuwania nafasi ya Udiwani wa Kata ya Ngokolo
kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Nyasani amechukua fomu hiyo asubuhi
katika ofisi za CCM kata ya Ngokolo, na kurejesha
rasmi siku ya leo, jambo lililowavutia watu wengi kushuhudia msanii na mtumishi wa umma akifanya
maamuzi ya kisiasa kwa ajili ya maendeleo ya jamii yake.
Mbali na taaluma yake ya ununuzi na
ugavi, Nyasani ni msanii wa Bongo Fleva anayezidi kujizolea mashabiki kutokana
na kazi zake zenye ubora na ujumbe mzito. Hivi karibuni ameachia wimbo wake
mpya uitwao “SAWA”, akiwa
amemshirikisha mkongwe wa muziki Mr.
Blue, wimbo ambao unaendelea kufanya vizuri kwenye majukwaa ya muziki
mtandaoni.





Post a Comment