Na mwandishi wetu
Kagera
Burchard Rwamtoga, mjasiriamali na mchumi ambaye ni mzaliwa wa kata ya Kasambya, Jimbo la Missenyi, amezidi kujipambanua na safari mpya ya kuwaletea maendeleo wana MISSENYI huku akitoa ahadi ya kupambana kwa nguvu na maarifa ili kuleta maendeleo ya kweli kwa wana Missenyi.
Katika mazungumzo na vyombo vya habari Rwamtoga anasema, anayo dhamira thabiti ya kuihudumia jamii.
Rwamtoga amesema ana dhamira ya kuleta mabadiliko chanya, hasa katika sekta za elimu na ajira na kwamba kama atapewa ridhaa ya kuongoza, atatumia ujuzi na uzoefu wake kuleta ufumbuzi wa kudumu kwa changamoto zinazowakabili wananchi, ikiwemo ufaulu usioridhisha wa wanafunzi na ukosefu wa ajira kwa vijana.
Rwamtoga anataja vipaumbele vyake na kusema kuwa, "Elimu ni msingi wa maendeleo hivyo lazima ahakikishe
watoto wanafanya vizuri katika masomo yao.
Amesema kuwa atajitahidi kuanzisha programu mbalimbali za kuwasaidia vijana kujiajiri wenyewe, ikiwa ni pamoja na kuwawezesha kupitia mafunzo ya ujasiriamali na ufundi.
Karibu Chuo cha Madini Shinyanga Earth Sciences Institute of Shinyanga (ESIS)
Mahali ambapo ubora ni msingi wetu na kila jiwe linachongwa kuwa hazina ya maarifa.
Unapojifunza hapa, haupati tu elimu ya vitabuni, bali pia maarifa ya vitendo yanayokujenga kuwa mtaalamu anayehitajika katika sekta ya madini, mafuta, na gesi.
Post a Comment