Timu ya Stand United imejipanga kikamilifu kwa mchezo wake wa Play Off dhidi ya Fountain Gate leo Ijumaa Julai 4, 2025, utakaopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kambarage, mjini Shinyanga.
Katika kuhamasisha ushindi wa timu hiyo, Mbunge wa Shinyanga Mjini, Mhe. Patrobas Katambi, ametoa motisha ya Shilingi Milioni Tano (5M) kwa wachezaji wa Stand United endapo watapata ushindi kwenye mchezo huo muhimu.
Mashabiki na wakazi wa Shinyanga wamehamasika kushuhudia mchezo huo wa kuvutia, ambao una nafasi ya kuamua mustakabali wa Stand United katika ngazi ya juu ya mashindano ya mpira wa miguu nchini.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment