Na Mapuli
Kitina Misalaba
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Ngokolo,
Victor Mkwizu, leo Julai 1, 2025, amerejesha rasmi fomu
yake ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuwania tena nafasi ya
udiwani wa kata hiyo katika uchaguzi mkuu ujao.
Mkwizu ambaye amehitimisha kipindi
chake cha uongozi wa miaka mitano, amesema ameamua kurejea tena kwa nia ya
kuendeleza misingi ya maendeleo aliyoweka pamoja na wananchi wa Ngokolo katika
kipindi kilichopita.
“Nimerudi kwa sababu bado nina ndoto
ya kuiona Ngokolo ikisonga mbele zaidi. Tumefanikisha mambo mengi, lakini bado
kuna mengi ya kufanya. Naamini kwa ushirikiano na wananchi, tunaweza,” amesema Mkwizu mara baada ya kurejesha fomu.
Ameongeza kuwa anayo dhamira ya
dhati ya kuendelea kutumikia wananchi kwa moyo wa uzalendo, huku akiahidi
kuzingatia maadili ya uongozi, ushirikiano na uwazi katika utekelezaji wa
majukumu.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment