" WASHINDI 20 WA KWANZA KATIKA KAMPENI YA ‘MIAMALA NI FURSA’ WAZAWADIWA

WASHINDI 20 WA KWANZA KATIKA KAMPENI YA ‘MIAMALA NI FURSA’ WAZAWADIWA


 Na Mwandishi wetu, Misalaba Media

Bank of Africa -Tanzania imetoa zawadi kwa washindi wake 20 wa kwanza wa wiki kupitia kampeni ya huduma za kibenki kwa njia ya kidigitali iitwayo “MIAMALA NI FURSA”, ambapo kila mmoja amepokea zawadi ya Sh50,000 kwa kutumia huduma za kibenki kwa njia ya simu za mkononi kupata huduma za huduma za kifedha.

Akizungumza kuhusu maendeleo ya kampeni hiyo iliyozinduliwa Juni 4, 2025, Afisa Mkuu wa Huduma za Kidigitali wa Bank of Africa-Tanzania, Bw Lameck Mushi, alisema kuwa mwezi mmoja tangu kuanza kwa kampeni hiyo ya miezi mitatu, imepokelewa vyema na umma wa Watanzania.

Bw Mushi alieleza kuwa kampeni hiyo inalenga kuhamasisha matumizi ya jukwaa la benki kupitia simu kwa kuwazawadia wateja wanaofanya miamala ya kila siku. Juhudi hizi ni sehemu ya dhamira ya benki yao kuendeleza matumizi ya huduma za benki kidigitali na kuendeleza ujumuishwaji wa kifedha nchini Tanzania.

“Tunafurahia mwitikio mkubwa tulioupokea hadi sasa. MIAMALA NI FURSA tayari imefanya huduma za kibenki kupitia simu kuwa za kuvutia na muhimu katika maisha ya kila siku ya wateja wetu,” alisema Bw Mushi.

Akiendelea, alisema ukweli kwamba “Wateja wanashinda zawadi za fedha kwa kufanya miamala ya kulipa bili au kutuma fedha unaonyesha kuwa vitendo vidogo, lakini vya mara kwa mara vina mchango mkubwa. Zaidi ya hapo, tumeongeza unafuu kwa wateja wetu kwa kupunguza ada za miamala ya Bank-to-Wallet kwa zaidi ya asilimia 50."

Kila wiki, wateja watano watakaokamilisha miamala mitatu ya Bank-to-Wallet (B2W) na muamala mmoja wa ziada (malipo ya bili, ununuzi wa muda wa maongezi au umeme) kupitia B-Mobile watakuwa na nafasi ya kushinda.

Mwisho wa kampeni hii, ambayo itaendelea hadi Septemba 2025, mshindi mkuu atajinyakulia zawadi ya pesa taslimu Sh5 milioni.

Afisa Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa RejaReja Asupya Nalingigwa, alisisitiza: “Lengo letu ni kufanya huduma za kibenki ziweze kufikiwa kwa urahisi, ziwe na manufaa na ziwaguse wateja wetu kwa ukaribu zaidi. Iwe uko mjini au kijijini, mradi una B-Mobile, unaweza kushiriki na kushinda.”

Ili kuhakikisha ushirikishwaji wa wote, Bank of Africa-Tanzania imehamasisha timu zake za matawi kote nchini kusaidia kuwaunganisha wateja wapya na kutoa mafunzo ya kutumia huduma hizo za kidigitali. Timu maalumu ya msaada wa kiufundi pia ipo tayari kusaidia kutatua changamoto zozote za upatikanaji na kuhakikisha uzoefu mzuri kwa watumiaji wote.

Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano Nandi Mwiyombella, aliongeza: “Kampeni hii si kuhusu zawadi pekee, bali ni kuhusu kuwapa nguvu wananchi. Kwa kuhamasisha matumizi ya huduma za kidigitali kwa njia shirikishi na rahisi, tunawasaidia Watanzania wengi zaidi kushiriki katika mfumo rasmi wa kifedha.”

Kwa zawadi zaidi za fedha na washindi wapya kutangazwa kila wiki, Bank of Africa -Tanzania inawaalika wateja wake wote kufanya miamala, kushinda, na kufurahia huduma za kibenki kwa urahisi kupitia simu zao.

 

 Kuhusu BOA Bank (T) Limited

BOA-Tanzania ni benki ya biashara binafsi inayotoa huduma kwa wateja wa kampuni kubwa, wateja wa kati (SME) na wateja wa rejareja nchini Tanzania. Ilianza shughuli zake Juni 2007 baada ya kununua Eurafrican Bank iliyokuwa ikifanya kazi nchini tangu Septemba 1995.

Benki hii ni sehemu ya kundi la Benki ya Afrika, ambalo lilianza shughuli zake mwaka 1982 nchini Mali.

Kundi hili linafanya kazi katika nchi 19 za Afrika, ikiwa ni pamoja na Afrika Magharibi, Afrika Mashariki, Afrika ya Kati, pamoja na ofisi za uwakilishi Paris (Ufaransa), Hispania, London (Uingereza) na China. Tangu mwaka 2010, Benki ya Afrika imekuwa chini ya umiliki mkubwa wa BMCE Bank, benki ya tatu kwa ukubwa nchini Morocco, inayotoa huduma katika nchi 31 na mabara 4.

Kwa sasa, BOA-Tanzania ina matawi 17 ya rejareja, yakiwemo 8 Dar es Salaam na 9 katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Zanzibar na miji mingine mikubwa.

Mawasiliano ya Vyombo vya Habari

Tovuti: www.boatanzania.com

Beatrice E. Mirigo – Maendeleo ya Bidhaa & Mawasiliano

Barua Pepe: beatrice.mirigo@boatanzania.co.tz

 

Simu: +255 699 000 260

Afisa Mkuu wa Huduma za Kidigitali wa Bank of Africa-Tanzania, Bw Lameck Mushi, akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu kampeni ya “Miamala ni Fursa” kwa wateja wao kwa kutumia huduma za kibenki kwa kupitia simu zao za kiganjani , kushoto ni Afisa Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa RejaReja Asupya Nalingigwa na kulia ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano Nandi Mwiyombella 

Post a Comment

Previous Post Next Post