" ALMASOUD KALUMUMA ATIMKIA ACT WAZALENDO KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA BUKOBA MJINI

ALMASOUD KALUMUMA ATIMKIA ACT WAZALENDO KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA BUKOBA MJINI

Na Lydia Lugakila 

Bukoba

Almsoud Dauda Kalumuna ameibuka tena katika ulingo wa siasa baada ya kukabidhiwa rasmi fomu ya kugombea ubunge kupitia chama cha ACT Wazalendo katika Jimbo la Bukoba Mjini.

 Hatua hiyo inamfanya kuwa mgombea halali wa chama hicho katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2025-2030

Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Bukoba Mjini, Melkion Komba, amethibitisha kuwa Kalumuna amekidhi vigezo vyote vya kisheria na tayari amekabidhiwa barua rasmi ya kuthibitisha kugombea.

 Komba alisisitiza kuwa mgombea huyo anatakiwa kujaza na kurejesha fomu hiyo kabla ya tarehe ya mwisho ya Agosti 27, 2025, kama inavyoelekezwa kwenye ratiba rasmi ya uchaguzi.

Akizungumza baada ya kupokea fomu yake, Kalumuna alisema kuwa ana dhamira ya dhati ya Ikuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wa Bukoba Mjini.

 Alitoa wito kwa wakazi wa jimbo hilo kuwa na ushirikiano huku  akiahidi kushirikiana nao katika kujenga uchumi na huduma bora za kijamii.

Kalumuna aliwahi kuwania nafasi hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo katika kura za maoni alipata kura 640 na kushika nafasi ya tatu akitanguliwa na mhandisi Johnston Mtasingwa ambaye sasa ni mgombea rasmi wa CCM kwa nafasi ya ubunge katika Jimbo la Bukoba Mjini.

GUSA LINK HAPA CHINI👇


🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post