Na Lydia Lugakila
Ngara
Mgombea ubunge wa Jimbo la Ngara mkoani Kagera, Dotto Jasson Bahemu, anatarajia kuchukua fomu ya kuipeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu ujao mwaka huu.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa, Dotto Bahemu atafanya shughuli mbalimba ambapo leo Agosti 26, 2025 kuanzia saa 3 asubuhi, msafara wa kumsindikiza utaanzia Murugarama na kuelekea Ofisi ya chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ngara.
Majira ya saa 4 asubuhi, matembezi yataanzia Ofisi ya chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ngara kuelekea mchakato wa kuchukua fomu katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya.
Aidha, kuanzia saa 5 asubuhi, Dotto Bahemu atarejea Ofisi ya CCM Wilaya ya Ngara kwa ajili ya kusalimia wanachama na kuomba udhamini.
Hatimaye, mnamo saa 7 mchana, ratiba hiyo itakamilika kwa msafara wa kuelekea Murugarama kwa ajili ya hitimisho.
GUSA LINK HAPA CHINI👇
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment