Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kisesa, nchini Tanzania, Luhaga Joelson Mpina amejiunga rasmi na Chama cha ACT Wazalendo, ambapo amesajiliwa kupitia mfumo wa kidijitali wa chama hicho ujulikanao kama ACT Wazalendo Kiganjani.
Usajili huo umefanywa na Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu, ambaye alimkaribisha rasmi Mpina na kumpa hadhi ya kuwa mwanachama wa chama hicho chenye mwelekeo wa kijamaa na kidemokrasia.

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Dorothy Semu, akimsajili Luhaga Joelson Mpina katika Mfumo wa ACT Wazalendo Kiganjani na kuwa mwanachama rasmi wa ACT Wazalendo.



Post a Comment