Na Mwandishi wetu, Misalaba Media
Hatimaye leo kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 u Ismail Ali Ussi, amefanya uzinduzi wa zahanati mpya na kugawa vifaa kinga kwa watu wenye ualbino,katika kata ya Ipilili wilayani nzega mkoani Tabora
Zahanati hiyo, iliyojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 103, ni moja ya miradi inayotekelezwa chini ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Ussi alisema kwamba jitihada za Serikali katika kusogeza huduma bora za afya kwa wananchi, hususan maeneo ya vijijini.
Alisema kuwa jitihada hizo zimegusa nyoyo za Watanzania wengi na kuleta matumaini mapya kwa Taifa.
Aidha Katika kuendeleza dhana ya usawa na kulinda afya za makundi maalum, Ussi alikabidhi vyandarua na vifaa kinga kwa watu wenye ualbino,kofia maalum za kujikinga na mionzi ya jua pamoja na mafuta ya kutunza ngozi .
Ussi alibainisha kwamba taaluma ya utabibu ilivyo ya kipekee kwa pongezi kwa madaktari na wataalam wa afya kwa moyo wao wa kujitolea na uzalendo wa hali ya juu.
“Kipekee nitaendelea kuwashukuru sana madaktari pamoja na walimu."
Alisema kwamba" hawa Wenzetu wanafanya kazi kwa uzalendo wa hali ya juu ya kuwahudumia wananchi bila ubaguzi Mungu amewajalia kuwa waadilifu, wazalendo na wanaojua kazi yao vizuri."
Uzinduzi wa zahanati ya Ipilili na utoaji wa vifaa hivyo unadhihirisha dhamira ya Mwenge wa Uhuru si tu kama alama ya ukombozi, bali pia kama chombo cha kuhamasisha maendeleo na usawa katika

Post a Comment