" THOMAS KITIMA ALIVYOANDIKA HISTORIA, AWAANGUSHA MIRAJI MTATURU NA NURSAT HANJE KURA ZA MAONI IKUNGI MASHARIKI — SASA JIMBO LIMETULIA

THOMAS KITIMA ALIVYOANDIKA HISTORIA, AWAANGUSHA MIRAJI MTATURU NA NURSAT HANJE KURA ZA MAONI IKUNGI MASHARIKI — SASA JIMBO LIMETULIA

Ikungi Mashariki, Singida —

Jimbo la Ikungi Mashariki limeandika ukurasa mpya katika historia ya siasa za ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya Thomas Mgonto Kitima, Mkurugenzi Mtendaji wa Chief Mgonto Foundation, kuibuka mshindi wa kwanza katika kura za maoni za ubunge zilizofanyika Agosti 4, 2025.

Kitima alipata kura 2,100, akimshinda kwa mbali aliyekuwa Mbunge anayemaliza muda wake Miraji Mtaturu aliyepata kura 1,111, pamoja na Nursat Shaaban Hanje, Mbunge wa Viti Maalum (CCM) aliyepata kura 1,918. Wote wawili walikuwa wakichuana naye kwenye mchakato huo wa kisiasa uliovuta hisia kubwa jimboni humo.

Ushindi wa Kitima umeelezwa na wachambuzi wa siasa kama wa kihistoria—sio tu kwa sababu aliwashinda viongozi wawili waliokuwa madarakani, bali pia kwa namna alivyojipambanua kupitia kazi yake ya kijamii na maendeleo kupitia Chief Mgonto Foundation. Wananchi wengi wamesema ushindi huo unaakisi kiu yao ya kupata mabadiliko halisi, usimamizi madhubuti wa rasilimali, na uongozi wa karibu na wananchi.

Kupitia taasisi hiyo, Kitima ameweza kufanikisha miradi mbalimbali ya afya, elimu, usaidizi kwa vijana, wanawake, pamoja na miradi ya maji na ujasiriamali — jambo lililompa heshima kubwa na kuaminika kwa wananchi wa kada mbalimbali.

Shangwe, vifijo, na matumaini vimetawala maeneo mbalimbali ya jimbo hilo mara baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, huku wananchi wakimpongeza kwa ushindi wake wa haki na wa wazi.

“Ushindi huu si wa mtu mmoja; ni wa wananchi wa Ikungi Mashariki. Tunaanza ukurasa mpya wa maendeleo, uwajibikaji, na mshikamano wa kweli,” alisema Kitima baada ya kutangazwa mshindi.

Kwa sasa, hali ya utulivu na mshikamano imerejea jimboni humo, ikiwa ni ishara ya kukubalika kwa mabadiliko mapya.

MATOKEO RASMI YA KURA ZA MAONI - IKUNGI MASHARIKI Tarehe ya uchaguzi: 04/08/2025 Idadi ya wapiga kura walioandikishwa: 9,868 Idadi ya kura zilizopigwa: 6,637 Kura zilizoharibika: 189 Kura halali: 6,448 Nafasi Jina Kamili Kura Alizopata 1 Thomas Mgonto Kitima 2,100 2 Nursat Shaaban Hanje 1,918 3 Miraji Jumanne Mtaturu 1,111 4 Emmanuel James Ithonde 772 5 Jonathan Andrew Njau 355 6 Mdimii Emmanuel Hongoa 192

Post a Comment

Previous Post Next Post