Askofu Mkuu Novatus Rugambwa, Mtanzania aliyewahi kuhudumu kama Balozi wa Baba Mtakatifu katika mataifa mbalimbali duniani, amefariki dunia usiku wa Septemba 16, 2025 akiwa mjini Roma, Italia, alikokuwa akiishi baada ya kustaafu utumishi wake wa kidiplomasia.
Taarifa za kifo chake zimetolewa na Redio Maria zikithibitisha kuwa Askofu Rugambwa alikuwa akipatiwa matibabu wakati wa umauti wake.
Askofu Rugambwa alizaliwa Oktoba 8, 1957 mkoani Kagera. Alipadrishwa Julai 6, 1986 na Askofu Nestorius Timanywa wa Jimbo Katoliki Bukoba (wakati huo). Baada ya miaka kadhaa ya huduma ya kipadre, alipewa daraja takatifu ya Uaskofu mnamo Machi 18, 2010, akiwekwa wakfu na Kardinali Tarcisio Pietro Evasio Bertone, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Vatican.
Katika safari yake ya utumishi, Askofu Rugambwa aliheshimika kwa nafasi alizoshika kama Balozi wa Baba Mtakatifu katika nchi mbalimbali, zikiwamo Angola, Honduras na visiwa vya Fiji. Alitambulika kwa mchango mkubwa katika kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia kati ya Vatican na mataifa hayo, pamoja na kuimarisha huduma ya Kanisa Katoliki duniani.
Post a Comment