" TUME YA HAKI ZA BINAADAM YAWANOA WAANDISHI WA HABARI ARUSHAKUELEKEA UCHAGUZI MKUU

TUME YA HAKI ZA BINAADAM YAWANOA WAANDISHI WA HABARI ARUSHAKUELEKEA UCHAGUZI MKUU

 Na Seif Mangwangi, Arusha. 

Tume ya Haki za binaadam na utawala Bora imewataka waandishi wa habari kutumia vizuri kalamu zao wakati wa kuripoti taarifa zao katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 2025.

Akifungua mafunzo ya siku Moja kwa waandishi wa habari Mkoa wa Arusha, kaimu Mwenyekiti wa Tume hiyo Mohamed Khamis Hamad amesema waandishi wa habari ni watu muhimu katika jamii hivyo taaluma hiyo inatakiwa kutumika vizuri.

Amesema waandishi wa habari wakitumia kalamu zao vibaya wataupotosha umma na kusababisha madhara makubwa kwa jamii ikiwemo kuleta machafuko ambayo matokeo yake ni kurudisha nyuma uchumi wa nchi jambo ambalo sio sahihi. 

Amesema katika kipindi Cha uchaguzi waandishi wa habari wanapaswa kuweka mizania Kwa wagombea wote ili kuepuka kutoegemea upande wowote.

Amewataka waandishi wa habari kuepuka kupokea rushwa kutoka kwa wagombea ili kuwapendelea katika taarifa zao jambo ambalo ni kinyume na maadili ya taaluma ya habari na Sheria za nchi.

Kwa upande wake mtoa mada katika mafunzo hayo Mohamed Bakari amesisitiza waandishi kuwa makini na kuzingatia sheria na taratibu, miiko na maadili katika utendaji kazi wao. 


"Katika kipindi hiki cha uchaguzi, waandishi wa habari wana wajibu wa kuhamasisha wananchi kupiga kura, kama Ibara ya 21 kifungu cha (1-2) inavyobainisha kuwa ni haki ya kila raia kushiriki uchaguzi. Epukeni upendeleo, usiri wa mtu pamoja na kumpiga picha mpiga kura katika chumba cha kupigia kura" Amesisitiza Bakari. 

Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Mwandishi wa habari wa Star TV na Radio Free Afrika aliyeshiriki mafunzo hayo Angelo Mwoleka amesema kila mwandishi azingatie kwanza usalama wake kazini, usalama wa nchi miiko na maadili ya uandishi.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post