
Na Lydia Lugakila, Misalaba Media Mbeya Mgombea wa udiwani kata ya Nsalaga Jimbo la Uyole mkoani Mbeya Clemence James Mwandemba ameahidi kuchapa kazi usiku na mchana ili kuiletea maendeleo ya haraka kata hiyo endapo atapata nafasi ya kuwatumikia wananchi. Mwandemba ametoa kauli hiyo Septemba 17, 2025 katika uzinduzi wa kampeini za udiwani kata ya Nsalaga. Akizungumza na Wananchi hao amesema atahakikisha anafanya kazi kwa bidii kama ilivyo kawaida yake huku akijitahidi kuwashirikisha viongozi na wananchi. Amesema kabla ya jukumu hilo amekuwa akifanya kazi za wananchi kwa kujitolea ambazo zimeleta maendeleo ndani ya kata hiyo. "Mtakumbuka hapa Nsalaga nilisimamia suala la mashamba na kuyakomboa yakabaki ya kwetu mmeona shule za kata hii zimefanyiwa ukarabati," alisema mgombea udiwani huyo. Amewaomba wananchi hao kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi(CCM) kwa kumpa kura nyingi Dkt. Tulia Ackson mgombea ubunge Jimbo la Uyole pamoja na Dkt. Samia Suluhu Hassan mgombea Urais kupitia tiketi ya chama hicho. Amesema Dkt. Samia ameleta shule mpya za msingi na sekondari pia zahanati hivyo wamchague kwa kila nyingi za kishindo.Hata hivyo, Mwandemba ameahidi kutoa fursa mbali mbali kwa watoto na vijana akina Mama ikiwa ni pamoja na kuwatetea wanyonge huku akimshukuru Rais Samia kwa namna alivyomuona kuwafaa wananchi pamoja na wajumbe waliofanya maamuzi.


🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment