" TISEZA yatembelea Kongani Maalum la Uwekezaji wa Buzwagi (SEZ)

TISEZA yatembelea Kongani Maalum la Uwekezaji wa Buzwagi (SEZ)

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) Bw.Gilead John Teri akizungumza na  Kamati ya Utekelezaji wa Kongani Maalum la Uwekezaji wa Buzwagi na Wafanyakazi wa Barrick baada ya kukamilisha ziara ya kikazi ya kutembelea eneo hilo.
Na Mwandishi Wetu, Misalaba MediaMamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) umeipongeza kampuni ya Barrick kwa weledi na kuzingatia viwango vya kimataifa katika mchakato wa ufungaji wa mgodi wake wa Buzwagi na kubadilisha matumizi ya eneo hilo na kuwa Kongani Maalum la Uwekezaji (SEZ) ambalo inafungua fursa za kiuchumi nchini.Mjumbe wa maofisa hao wa TISEZA ukiongozwa na Mkurugenzi  Mkuu wake, Gilead John Teri ilifanya ziara hiyo kikazi jana na kuridhishwa na mchakato mzima wa ufungwaji wa mgodi huo Akiwa katika eneo hilo , Bw Teri alipata taarifa fupi ya uwekezaji wa aina mbalimbali ndani ya kongani hilo maalum la Uwekezaji (SEZ) na kukagua maeneo mbalimbali yatakayotumiwa na wawekezaji watakaohitaji kuwekeza katika Kongani hiyo na alitembelea kiwanda cha kuzalisha (Conveyor) ambacho tayari kimeanza kufanya uzalishaji na kutoa fursa za ajira.Akiongea baada ya ziara hiyo,Bw.Teri alitoa pongezi kwa kampuni ya Barrick nchini kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za serikali kwa kufanikisha ufungaji wa mgodi huo kwa  viwango vya kimataifa na kufungua fursa ya eneo la kimkakati wa kukuza uchumi kupitia uanzishaji wa viwanda na kufungua milango ya biashara.“Nawapongeza Barrick kwa kuhakikisha mgodi huu unafungwa kitaalamu pia nachukua fursa hii kuwashukuru kamati ya Utekelezaji wa Kongani hii inavyofanya kazi kwa Kushirikiana na mamlaka mbalimbali lengo likiwa kutimiza kufanikisha lengo la serikali la kuhakikisha eneo hili linatumika kimkakati ili liweze kuleta matokeo chanya kwa taifa ”,alisema Teri.Teri pia alisema ameridhishwa na utangazaji wa eneo hilo unaoendelea ambazo zinabainisha fursa zilizopo na mipango iliyowekwa na serikali kwa ajili ya kutoa huduma kwa kuhakikisha zinapatikana katika eneo moja (One Stop Centre).Kwa upande wake Meneja wa ufungaji wa Mgodi wa Barrick Buzwagi, Mhandisi Zonnastral Mumbi alisema tayari eneo hilo la kongani ya Buzwagi limepatiwa usajili na serikali kwa ajili ya shughuli hiyo maalum ambapo ukamilikaje wake utachochea ukuaji wa uchumi na ajira kwa vijana hapa nchini.Aidha Mumbi alieleza ujumbe huo kuwa hadi kufikia sasa wawekezaji  19 wameonyesha nia ya Kuwekeza katika Kongani hiyo huku wawekezaji tano  tayari wameanza mchakato wa usajili na tayari mwekezaji mmoja ameanza uzalishaji .Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,  Mboni Mhita, alitoa wito  kwa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) kuweka msisitizo katika kutangaza mradi mkubwa wa Kongani  Maalum la Uwekezaji wa Buzwagi ( SEZ) ambao unatarajiwa kuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya kiuchumi kwa Mkoa na Taifa kwa ujumla.Aidha,  RC Mboni alibainisha  kuwa Shinyanga ipo tayari kupokea wawekezaji kutokana na mazingira wezeshi yaliyowekwa na serikali pamoja na Mkoa kuwa na rasilimali zote muhimu kwa uwekezaji ikiwemo ardhi, upatikanaji wa maji, umeme, miundombinu ya kisasa ikiwa pamoja na barabara, uwanja wa ndege wa Shinyanga na Kahama, mtandao wa mawasiliano, na  nguvu kazi.Meneja wa ufungaji Mgodi wa Barrick Buzwagi, Mhandisi Zonnastral Mumbi akifafanua jambo kwa ujumbe kutoka Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) jinsi mchakato  wa kubadilisha mgodi huo uliofungwa  kuwa  Kongani ya Buzwagi unavyoendlea  wakati ulipofanya ziara kwenye eneo hilo la mgodi.Meneja wa ufungaji Mgodi wa Barrick Buzwagi, Mhandisi Zonnastral Mumbi (aliyenyoosha mkono)  akiwatembeza ujumbe kutoka Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Kongani Maalum la Uwekezaji wa  Buzwagi.  Meneja Utekelezaji wa Mradi  wa Kongani ya Buzwagi  kutoka Barrick, Stanley Joseph akifanya wasilisho kwa ujumbe wa maofisa waandamizi kutoka Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) uliofanya ziara mgodini hapo.Ujumbe kutoka Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) ulipata fursa kutembelea maeneo ya wawekezaji mbalimbali kwenye eneo la Kongani Maalum la Uwekezaji wa Buzwagi.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post