" DKT. TULIA ACKSON AZINDUA KAMPENI ZA UBUNGE JIMBO LA USHETU UMATI MKUBWA WAJITOKEZA

DKT. TULIA ACKSON AZINDUA KAMPENI ZA UBUNGE JIMBO LA USHETU UMATI MKUBWA WAJITOKEZA

Na Lydia Lugakila, Misalaba Media Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Dkt. Tulia Ackson, amezindua rasmi kampeni za Ubunge wa Jimbo la Ushetu kupitia chama Cha mapinduzi (CCM).Uzinduzi huo umefanyika Septemba 18 katika viwanja vya Shule ya Msingi Ibelasuha, Ushetu mkoani Shinyanga. Hafla hiyo ilihudhuriwa na umati mkubwa wa wanachama wa chama hicho, pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali wa CCM. Wakati wa uzinduzi, Dkt. Ackson amesisitiza umuhimu wa kuungwa mkono kwa mgombea ubunge, Ndg. Emmanuel Cherehani, akisema kuwa ni lazima watanzania wajitokeze kupiga kura ili kuhakikisha viongozi wema wanachaguliwa.Aidha, Spika alitumia fursa hiyo kuzungumzia mipango ya maendeleo ya Jimbo la Ushetu ambayo inatarajiwa kuboresha maisha ya wananchi, akiwemo kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia programu zinazokuza ujasiriamali. Dkt. Ackson ameahidi kuimarisha ushirikiano kati ya serikali na wananchi ili kujenga jamii yenye maendeleo endelevu.Katika hotuba yake, Ndg. Cherehani alieleza mikakati yake ya kutatua changamoto zinazowakabili wananchi, akitaja elimu, afya, na ajira kama maeneo muhimu yenye kipaumbele.Amewasihi wapiga kura kuhakikisha wanachagua viongozi wenye maono na dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi. Katika hafla hiyo, Madiwani wa Jimbo la Ushetu walikumbushia umuhimu wa umoja na mashirikiano katika kuleta maendeleo na kuahidi kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Dkt. Tulia Ackson, akimuombea kura nyingi za ndiyo mgombea ubunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani. 



🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

 

Post a Comment

Previous Post Next Post