Na.Mwandishi wetu
Mwandishi wa habari mkongwe na Mwandamizi Edwin Soko ametoa rai Kwa waandishi wa habari kuelekea uchaguzi mkuu kuzingatia sheria, kanuni na weledi wanapotimiza majukumu yao kuelekea uchaguzi mkuu.
Soko amesema hayo wakati aliipohojiwa na Vyombo mbalimbali kufuatia kushikiliwa kwa baadhi ya waandishi kwa makosa ya kumiliki Vyombo vya habari vya mtandaoni bila kusajiliwa.
Soko ameonyesha masikitiko yake Kwa baadhi ya waandishi hasa waandishi wa habari wachanga wanaoangukia kwenye mikono ya Polisi kwa kutozijua sheria za Nchi.
Soko amewakumbisha waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari vya mtandaoni kuzingatia matakwa ya kisheria kwa kusajili vyombo hivyo kama inavyoelekezwa na Kanuni ya 4(1) ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni za mwaka 2020. Kufanya hivyo kutawasaidia kuepuka usumbufu usio wa lazima kutoka Kwa vyombo vya dola, ikiwemo Jeshi la Polisi.
" Mwandishi wa habari anaposhikiliwa kwa Mamlaka za Nchi Kwa siku kadhaa kuna athari za kisaikolojia anazopata lakini pia kupunguza uwajibikaji kwenye kuihabarisha jamii. Alisema Soko
Pia Soko ameiomba Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kufikiria upya ada ya kusajili chombo Cha Habari Cha mtandaoni(Blog) ili kuwawezesha waandishi wa habari kumudu gharama za kusajili kwani kiwango kikubwa Cha ada ya usajili kinatoa mwanya wa baadhi yao kumiliki Vyombo hivyo bila kusajili.
Soko pia ametoa rai Kwa waandishi wa habari wote kufanya kazi Kwa weledi na kuweka mbele maslahi ya watanzania.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment