" FARIS AWATAKA VIJANA KUSIMAMA KISAWA SAWA KATIKA KUIUNGA MKONO SERIKALI

FARIS AWATAKA VIJANA KUSIMAMA KISAWA SAWA KATIKA KUIUNGA MKONO SERIKALI

Na Lydia Lugakila, Misalaba Media 

Kagera 

Mwenyekiti wa umoja wa vijana (UVCCM) mkoa wa Kagera Faris Buruhan amewataka vijana mkoani Kagera kuiunga mkono Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana ilivyoleta maendeleo hasa katika mkoa wa Kagera na kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Faris ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mbio za mwenge wa uhuru eneo la manispaa ya Bukoba mkoani humo.

 Amesema kuwa vijana wanatakiwa Kuiunga mkono Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutambua mema na mazuri aliyoyafanya Mhe, Dokta. Samia  Suluhu Hassan kwa kipindi chote cha uongozi wake.

Ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya sita imeleta maendeleo mengi katika mkoa wa Kagera ikiwemo kuwapa Kipaumbele kikubwa ikiwemo  kuwawezesha  katika kilimo,ufugaji pamoja na ufundi.

Hata hivyo amesema kuwa vijana wa mkoa wa kagera wapo tayari kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu mwaka huu ambao unatarajiwa kufanyika mwaka huu huku akiwataka vijana hao kukichagua chama cha Mapinduzi ambacho kitawaletea viongozi bora ambao wataleta maendeleo makubwa  Nchini.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post