Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita
imeendelea kutoa huduma za bure za upimaji wa macho, masikio na magonjwa
mbalimbali katika maonesho ya teknolojia ya madini yanayofanyika mkoani humo,
ambayo yanatarajiwa kufungwa leo.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Mfaume
Kibwana, alisema kushiriki kwao maonesho hayo kwa mwaka wa tatu mfululizo
ni sehemu ya kuthamini na kutambua mchango wa wananchi, hivyo wameamua
kurudisha kwao kwa kuwapatia huduma muhimu za kiafya bila malipo.
“Mwamko wa wananchi ni mkubwa sana,
wengi wanakuja kupata huduma. Tunashauri waendelee na utamaduni wa kupima afya
zao mara kwa mara,” alisema Kibwana.
Naye Daktari Bingwa wa Macho, Gloria
Andrew, alisema changamoto kubwa kwa wakazi wengi wa Geita ni aleji ya
macho, hali inayosababishwa zaidi na vumbi katika mazingira ya mkoa huo.
Alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kupima macho mapema na kuchukua tahadhari
ili kuepuka madhara zaidi.
Hospital hiyo pia imepewa tuzo ya mshindi wa kwanza kwa taasisi za afya ambazo zinatoa huduma .
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment