" SIMBA SC YATINGA RAUNDI YA PILI LIGI YA MABIGWA AFRIKA

SIMBA SC YATINGA RAUNDI YA PILI LIGI YA MABIGWA AFRIKA







Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wamefanikiwa kufuzu hatua inayofuata ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Gaborone United ya Botswana katika mchezo wa marudiano uliochezwa leo, Septemba 28, 2025, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Simba walipata bao la kuongoza dakika ya 43 kupitia kwa Jean Charles Ahoua kwa mkwaju wa penalti, kufuatia shambulizi lililosababisha mchezaji wa Gaborone kufanya madhambi ndani ya eneo la hatari.

Hata hivyo, dakika ya 66, Gaborone walisawazisha kupitia nahodha wao Lebogang Ditsele, naye pia akiandika jina lake kwenye bao hilo kwa mkwaju wa penalti.

Kwa matokeo haya, Simba SC wanasonga mbele kwa jumla ya mabao 2-1, baada ya kushinda mchezo wa kwanza ugenini kwa bao 1-0.

Ni hatua muhimu kwa Wekundu wa Msimbazi, ambao sasa wanajiandaa kwa changamoto za raundi ya pili wakiwa na matumaini ya kufanya vizuri msimu huu katika michuano hiyo kabisa barani Afrika baada ya msimu uliopita katika Kombe la Shirikisho kufika hatua ya fainali.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post