Na: Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
Katika kuhakikisha wale wote wenye nia ya kuwasilisha maombi yao ya mikopo ya elimu ya kati na ya juu wafanikiwa bila kikwazo, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeongezeka muda wa maombi ya uombaji mikopo kutoka Agosti 31, 2025 hadi Septemba 14, 2025.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dkt. Bill Kiwia, katika taarifa yake kwa waombaji mikopo na Umma. Dkt. Kiwia amesisitiza uamuzi wa kuongeza muda wa wiki mbili (siku 14) unatokana na kuwepo baadhi ya waombaji mikopo kushindwa kuwasilisha na kukamilisha maombi yao ndani ya muda uliotolewa awali kuanzia Juni 15 hadi Agosti 31, 2025.
Hivyo basi, HESLB imeona haja ya kuongeza muda hadi Septemba 14 ili wale wote walioshinda kukamilisha maombi yao waweze kukamilisha ili wanufaika na fursa ya mikopo ya elimu inayotolewa na serikali.
Kimsingi, hadi kufika Agosti 31, 2025, HESLB imefanikiwa kupokea maombi ya mikopo 157,309 huku maombi ya Ufadhili wa Samia "Samia Scholarships" yakiwa yamefikia 960 ambapo wito umetolewa wa wale wote ambao hawajafanikiwa kuwasilisha maombi yao kutumia vyema muda wa ziada ulioongezwa kwani baada ya hapo hakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza.
Post a Comment