Na Osama Mohamedi chobo, Misalaba Medi -LindiChangamoto ya wanyama wakali pamoja na hali duni ya barabara bado ni kikwazo kwa wakazi wa Wilaya ya Kilwa, licha ya jitihada kubwa zilizofanywa na serikali kuboresha miundombinu hiyo.Hayo yamebainika wakati wa ziara ya mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, mkoani Lindi, ambapo alikutana na wananchi wa jimbo la Kilwa Kaskazini.Akizungumza katika mkutano huo, mgombea ubunge wa jimbo hilo, Mheshimiwa Kinjekitile Ngombale-Mwiru, amesema kuwa pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya miundombinu, bado kuna maeneo ambayo yanahitaji msukumo zaidi, hususan barabara zinazoelekea vijijini.> “Tunaipongeza serikali kwa kazi kubwa iliyoifanya kuboresha miundombinu, lakini bado tuna changamoto kubwa ya barabara vijijini pamoja na wanyama wakali wanaoathiri shughuli za wakulima na wafugaji,” alisema Mh. Ngombale-Mwiru.Aidha, alisisitiza kuwa ili kuharakisha maendeleo ya wananchi wa Kilwa na kuongeza kasi ya uchumi wa eneo hilo, ni muhimu serikali ikaongeza juhudi katika kuboresha barabara, hasa wakati huu wa mvua ambapo maeneo mengi hayafikiki kirahisi.Ziara ya Dkt. Samia mkoani Lindi ni sehemu ya kampeni zake kuelekea uchaguzi mkuu, ambapo pamoja na kusikiliza kero za wananchi, amekuwa akieleza mipango ya serikali ya awamu ijayo endapo atapewa ridhaa ya kuongoza tena.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment