" TYC YATANGAZA NAFASI YA KAZI YA OFFICE ASSISTANT SHINYANGA

TYC YATANGAZA NAFASI YA KAZI YA OFFICE ASSISTANT SHINYANGA

TANGAZO LA KAZI – MSAIDIZI WA OFISI

UTANGULIZI

 Tanzanian Youth and Children (TYC) ni Asasi Isiyo ya Kiserikali (NGO).

 Asasi hii ilianzishwa kama CBO mwaka 2017 na ilisajiliwa kikamilifu Aprili, 2022 na kupewa mamlaka ya kufanya kazi Tanzania Bara. Lengo letu ni kukuza na kutetea jamii ili kuhakikisha familia zao zinakuwa huru na vikwazo vya kijamii na kiuchumi na kufikia uwezo wao kamili katika maisha yao.

TYC inatafuta Msaidizi wa Ofisi atakayehusika na shughuli za kila siku za uendeshaji. Ikiwa unaona unaweza kushiriki katika majukumu yaliyotajwa, unakaribishwa kujiunga na timu yetu.

MSAIDIZI WA OFISI:

  • Idadi ya nafasi: Moja (1)
  • Eneo la kazi: Manispaa ya Shinyanga
  • Mshahara: Kifurushi cha kuvutia

Msaidizi wa ofisi atakuwa na jukumu la kufanya kazi mbalimbali za kiutawala na za kiofisi kusaidia shughuli za kila siku.

Majukumu na Wajibu

  • Kusimamia kazi za kiofisi kama kupanga na kutuma barua pepe/nyaraka
  • Kuhifadhi na kuorodhesha vifaa vya ofisi na kuagiza vipya inapohitajika
  • Kuwakaribisha wageni ofisini
  • Kujibu simu
  • Kuhakikisha ofisi inaendeshwa kwa ufanisi
  • Kupanga ratiba za mikutano na kutuma mialiko ya vikao kwa washiriki
  • Kuwakilisha na kuhudhuria mikutano kwa ajili ya kuchukua kumbukumbu/makabrasha ya kikao
  • Kufanya shughuli nyingine yoyote rasmi zitakazoelekezwa na msimamizi/mwajiri

Sifa na Vigezo vya Mwombaji

  • Elimu ya kuanzia kidato cha nne na kuendelea katika masomo ya Uhazili, Maendeleo ya Jamii, Rasilimali Watu, Mipango ya Miradi, Kazi za Jamii, Teknolojia ya Habari au fani nyingine zinazohusiana.
  • Awe na uwezo wa kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja na kuwa na nidhamu ya kupanga ratiba za watu wengine.
  • Uwezo wa kompyuta za msingi
  • Uwezo wa kubadilika na kuweka vipaumbele kwenye kazi mpya zinapojitokeza
  • Uwezo wa mawasiliano ya kijamii
  • Ujuzi wa usimamizi wa muda
  • Ustadi wa kuhudumia wateja

ANGALIZO: Usilipe fedha yoyote kwa tangazo hili. TYC inakataza aina yoyote ya rushwa kuhusiana na nafasi hii. Tunaamini katika uadilifu, uwezo na ubunifu wa waombaji.

Tuma barua ya maombi, CV na vyeti vya kitaaluma kabla ya tarehe 30 Septemba, 2025. Ni waombaji walioteuliwa pekee watakaowasiliana.

Wanawake wanahimizwa kuomba wenye umri wa miaka 18 hadi 27. Tunakubali maombi kwa njia ya mtandao pekee kupitia barua pepe. Waombaji wanaoishi Shinyanga watapewa kipaumbele.

Tuma kupitia barua pepe: tycnew@gmail.com

Anuani:

 Mkurugenzi Mtendaji

 Tanzanian Youth and Children (TYC)

 S.L.P 1362, Shinyanga-

Tanzania

 

Post a Comment

Previous Post Next Post