" LITTLE TREASURES NURSERY & PRIMARY SCHOOL YAFANYA MAHAFALI YA 14 YA AWALI NA YA 9 YA DARASA LA SABA

LITTLE TREASURES NURSERY & PRIMARY SCHOOL YAFANYA MAHAFALI YA 14 YA AWALI NA YA 9 YA DARASA LA SABA

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Meki C. Joseph, amesema Little Treasures, akisoma taarifa fupi ya shule.

Shule ya Little Treasures Nursery & Primary School imefanya mahafali yake ya 14 kwa wanafunzi wa elimu ya awali na ya 9 kwa darasa la saba, ambapo jumla ya wahitimu 164 wameaga rasmi hatua zao za masomo.

Sherehe hizo zimefanyika Septemba 20, 2025 katika viwanja vya shule hiyo vilivyopo Kijiji cha Bugayambelele, Kata ya Kizumbi, Manispaa ya Shinyanga, zikihudhuriwa na wazazi, walimu pamoja na wageni mbalimbali.

Mgeni rasmi Mthibiti Ubora wa Shule katika Manispaa ya Shinyanga Samson Nyanda, ambaye alikuja kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro.

Akisoma taarifa fupi ya shule, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Meki C. Joseph, amesema Little Treasures ilianza mwaka 2011 ikiwa ni shule ya awali ndogo kwenye nyumba ya kupanga, na baadaye mwaka 2014 ikahamia kwenye majengo yake ya kudumu. Kwa sasa shule inatambulika rasmi na Wizara ya Elimu chini ya usajili namba EM 15841.

Mwalimu Joseph ameongeza kuwa shule hiyo inajivunia utoaji wa huduma bora ikiwa ni pamoja na usafiri wa wanafunzi, mabweni ya kisasa, usalama wa watoto, lishe bora, walimu wenye sifa stahiki na huduma za afya kupitia Luckmed Polyclinic, ambapo madaktari bingwa wa watoto huhudumia wanafunzi na jamii inayowazunguka.

Katika mahafali hayo, jumla ya 65 wamehitimu elimu ya awali (wavulana 26 na wasichana 39), huku darasa la saba likitoa wahitimu 99 (wavulana 50 na wasichana 49).

“Kwa jumla leo tunasherehekea wahitimu 164, wote wakiwa wameandaliwa kitaaluma, kiuzalendo na kimaadili,” ameeleza Mwalimu Joseph katika taarifa yake.

Mwalimu Joseph ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wazazi wote wanaotoa ushirikiano unaowezesha maendeleo ya watoto wao.

Aidha, amewatangazia wazazi kuhusu Little Treasures Secondary School, shule ya sekondari ya jirani ambayo imekuwa ikifanya vizuri kitaifa. Mwaka uliopita, kati ya watahiniwa 58 wa kidato cha nne, 41 walipata Division One na wengine 17 Division Two.

Akihutubia kwa niaba ya mgeni rasmi, Samson Nyanda ameupongeza uongozi wa shule hiyo kwa kazi kubwa ya kulea na kusomesha watoto katika mazingira bora.

Amesema shule hiyo imekuwa mfano wa kuigwa katika Manispaa ya Shinyanga kutokana na nidhamu ya wanafunzi, ubunifu wa walimu na ufaulu unaoonekana mwaka hadi mwaka.

Ameongeza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na shule binafsi zinazotoa mchango mkubwa katika sekta ya elimu kwa kuhakikisha ubora na viwango vinazingatiwa ili watoto wa Kitanzania wapate elimu bora.

Mkurugenzi wa Shule ya Little Treasures Lucy Dominic Msele, ameushukuru uongozi wa Serikali, wazazi na jamii kwa kuendelea kushirikiana na shule hiyo ambapo amesema mafanikio ya shule yamejengwa kwa mshikamano kati ya walimu, wazazi na wanafunzi, jambo linaloifanya Little Treasures kuwa na matokeo chanya kila mwaka.

Lucy ameeleza kuwa shule itaendelea kusimamia maadili mema, nidhamu na ubora wa elimu kwa lengo la kuwaandaa watoto kuwa viongozi wa baadaye wanaoweza kubadilisha dunia.

Kwa upande wake, Meneja wa Shule Shule ya Little Treasures ya Wilfred Mwita, amewahimiza wazazi kuhakikisha watoto wanapewa mahitaji muhimu ya shuleni na msaada wa karibu hata wanapokuwa nyumbani ili kuendeleza mafunzo wanayoyapata shuleni huku akitaja kuwa mchango wa wazazi ni nguzo muhimu katika kufanikisha ufaulu na malezi bora ya watoto.

Meneja huyo ameongeza kuwa shule inaendelea kuboresha miundombinu na huduma mbalimbali ili watoto wapate mazingira bora zaidi ya kujifunza na kujilea kimaadili.

Baadhi ya wahitimu wamewashukuru walimu wa shule hiyo kwa malezi na elimu waliyopewa, huku wakiwahakikishia wazazi na walimu kuwa watafanya vizuri katika mitihani yao ya Taifa. Wamesema nidhamu, misingi ya maadili na elimu waliyopewa Little Treasures itawasaidia kufanikisha ndoto zao.

Shule ya Little Treasures inaongozwa na kauli mbiu:
“Prepare to Change the World”

Wanafunzi wahitimu wakifanya maandamano ya amani mjini Shinyanga ikiwa ni sehemu ya mahafali yao.Wanafunzi wahitimu wakifanya maandamano ya amani mjini Shinyanga ikiwa ni sehemu ya mahafali yao.Wanafunzi wahitimu wakifanya maandamano ya amani mjini Shinyanga ikiwa ni sehemu ya mahafali yao.

Mgeni rasmi na viongozi mbalimbali wakiwasili katika eneo la mahafali.






Mkurugenzi wa Shule ya Little Treasures Lucy Dominic Msele.

 

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post