" SHIRIKA LA WOMEN IN NATURE TANZANIA LAAHIDI KUKISAIDIA KIKUNDI CHA FURSA WOMEN

SHIRIKA LA WOMEN IN NATURE TANZANIA LAAHIDI KUKISAIDIA KIKUNDI CHA FURSA WOMEN

Na Tonny Alphonce -Misalaba MediaKikundi Cha Fursa Women Group Cha Buhongwa mkoani Mwanza kimeomba kusaidiwa mashine za kisasa Ili ziweze kuwasaidia katika kazi yao ya Uchakataji wa Samaki na Dagaa.Mwenyekiti wa kikundi hicho Fatuma Katulla amesema Kwa Sasa wanaendelea na kazi hiyo ya Uchakataji lakini changamoto kubwa ni wakati wa mvua Dagaa wengi wanaharibika."Tunahitaji mashine ya kisasa ya kukaushia Dagaa Ili tusipate changamoto wakati wa mvua maana mvua ikipiga siku mbili mfululizo Dagaa wanatuozea na tunapata hasara kubwa"alisema FatumaFatuma amesema Ili pia waweze kushindana katika soko la kimataifa wanahitaji vifungishio vya kisasa pamoja na box maalumu za kusafirishia Dagaa na Samaki"Kwa Sasa bidhaa yetu inakosa vifungashio maalumu hivyo inatuwia vigumu pia katika kujitangaza"alisema FatumaAkizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda Cha Fursa Women Group mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Women in Nature Dr Anna Mahullu amesema wataangalia namna gani ya kutatua changamoto zinazo kikabiri kikundi hicho"Kwanza niwapongeze sana kikundi Cha Fursa Women maana kazi yenu mnaifanya Kwa usafi na Kwa kiwango Cha Hali ya juu,sisi Kwa kushirikiana na Wadau wengine tutaangalia namna gani ya kuwatatulia baadhi ya changamoto.Nae mratibu wa shirika la Sustainable Future Tanzania Lewis Ismail amekipongeza kikundi hicho kwa namna kinavyofanyakazi ya Uchakataji wa Samaki pamoja na utunzaji wa Mazingira.Kikundi Cha Fursa Women kina wanachama 22 kikifanya shughuli zake Buhongwa mkoani Mwanza.

 

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post