

NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wameanza kampeni yao ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kishindo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Fountain Gate FC, katika mchezo uliopigwa leo, Septemba 25, 2025, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Simba SC walitangulia kupata bao la mapema dakika ya 6 kupitia kwa beki wao wa kati raia wa Afrika Kusini, Rushine De Reuck.
Dakika ya 37, kiungo mshambuliaji machachari kutoka Ivory Coast, Jean Charles Ahoua, aliongeza bao la pili na kuzamisha matumaini ya wapinzani wao kabla ya mapumziko.
Kipindi cha pili Simba wakidhibiti mchezo, na dakika ya 58, mshambuliaji hatari raia wa Ghana, Jonathan Sowah, alifunga bao la tatu na kuzima kabisa matumaini ya Fountain Gate kurejea mchezoni.
Ushindi huu mnono unaifanya Simba SC kuanza msimu kwa pointi tatu muhimu, huku wakionesha dhamira ya kweli ya kurejesha taji la Ligi Kuu msimu huu.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment