Mkuu wa Idara ya maliasili na hifadhi ya mazingira Manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga akitoa mada kuhusiana na utunzaji wa mazingira kwa wajumbe wa Kamati za mazingira kutoka Kata ya Ndala na Masekelo ambayo yameandaliwa na Shirika la YAWE
Kamati za Mazingira ngazi ya Kata zimetakiwa kuhakikisha zinatumia sheria ya mazingira kudhibiti uharibifu wa mazingira unaofanywa kwenye maeneo mbalimbali ili kulinda mazingira yasiendelee kuharibiwa kutokana na shughuli za kibinadamu zinazoendelea.
Hayo yameelezwa leo Mkuu wa Idara ya maliasili na hifadhi ya mazingira Manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga wakati wa mafunzo kwa wajumbe wa Kamati za mazingira kutoka Kata ya Masekelo na Ndala,ambayo yameandaliwa na Shirika la YAWE ili kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati za Mazingira.
Amesema kamati hizo zinatakiwa kwenda kusimamia mazingira kwa nguvu zote kutokana na kuwepo uharibifu mkubwa ikiwa ni pamoja na kuchukuwa hatua kwa watu wanaolima kandokando ya mito na kwenye vyanzo vya maji.
“Wajibu wa kulinda mazingira ni wa kila mtu maana mazingira yanapoharibiwa kuna athari kubwa zinatokea hivyo kwa kutumia sheria ya mazingira ya mwaka 2004 kamati hizi sasa zinatakiwa kwenda kufanya kazi kwa bidii kubwa”amesema Manjerenga



Mratibu wa Mradi wa Uendelezaji wa Miji na Majiji TACTIC Mhandisi Kassim Thadeo amesema ili kulinda usalama wa wananchi na watumiaji wa Barabara ya Ndala kwenda Hospitali ya Mwawaza wakati ujenzi ukianza ,wataweka alama mbalimbali za barabara kwenye sehemu zenye uhitaji na sehemu ambazo kuna shule.
Amesema katika ujenzi wa barabara wanazingatia huduma zote muhimu vikiwemo vivuko na kuweka mazingira vizuri baada ya ujenzi kukamilika zikiwemo sehemu ambazo walikuwa wanachukuwa moramu na kwa ajili ya ujenzi.

Post a Comment