" WANANCHI MKOANI MBEYA WAHIMIZWA KUFANYA UCHUNGUZI WA AFYA ZAO MARA KWA MARA ILI KUEPUKA MAGONJWA YASIYO YA LAZIMA

WANANCHI MKOANI MBEYA WAHIMIZWA KUFANYA UCHUNGUZI WA AFYA ZAO MARA KWA MARA ILI KUEPUKA MAGONJWA YASIYO YA LAZIMA

Na Lydia Lugakila MbeyaMkoa wa Mbeya ni moja ya mikoa yenye  chakula cha kutosha licha ya kuwepo na tatizo la baadhi ya watu kutozingatia kula mlo kamili na wengine kutokula kwa wakati.Misalaba media imefunga safari hadi kituo cha matibabu kijulikanacho kama THE BIG MIRACLE HERBAL CLINIC cha tiba lishe na tiba mbadala kilichopo eneo la Kabwe block T. Barabara ya madaraka.Akizungumza juu ya elimu ya Afya na huduma hiyo mapema Septemba 9, 2025 Dr. Yuston Magolodi amesema kuwa watu mengi wamekuwa hawazingatii namna bora ya ulaji huku wengine wakiwa hawafanyi uchunguzi wa  afya zao mara kwa mara jambo ambalo limeonekana kuwatesa wengi.Dr. Magolodi amesema  vijana wenye umri wa miaka 15- 35 Mkoani Mbeya wanakumbwa na tatizo la vidonda vya tumbo kuliko magonjwa mengine huku sababu ikitajwa kuwa baadhi yao wamekuwa hawana ratiba nzuri ya kula chakula huku wengine wakila chini ya kiwango na wengine kutokujenga mazoea ya kupima Afya zao jambo ambalo amelitaja kama ni hatari."Nawaombeni wananchi mjenge mazoea ya kupima Afya mara kwa mara mfano ukiangalia watu wazima kuanzia miaka 35 wamekumbwa na matatizo yakiwemo ya mifupa, maumivu ya viungo hata wengine kudiliki kutopima Afya zao"alisema Dr Magolodi.Aidha ameongeza kuwa tayari baadhi ya watu wamepoteza  virutubisho, wamepungukiwa vitamini, na madini kutokana na ulaji usio mzuri hali inayosababisha watu kuwa na maumivu ya mifupa, viungo na pingili za uti wa mgongo.Ameongeza kuwa Wazazi wanatakiwa kuwapa watoto chakula chenye viwango kwani watoto walio wengi wamekuwa hawapati chakula cha kutosha na baadhi kutokufanyiwa vipimo mara kwa mara.Aidha amesema magonjwa mengi yanayowasumbua watu ukubwani ni yale watu waliyoyapata wakiwa katika ujana. Amewahimiza wananchi Mkoani Mbeya kujitokeza kwa wingi kupima Afya zao katika kutuo hicho cha The big miracle ClinicAmeongeza kuwa kituo hicho kinapokea wagonjwa wa kila aina ambapo ukifika hapo unafanyiwa uchunguzi wa mwili mzima bila gharama jambo ambalo limewavutia wengi kwani ni tofauti na vituo vingine vya namna hiyoKituo hicho kinajishughulisha na matibabu ya binadamu ambapo kinatumia dawa  zinatokana na vyakula,  mimea , maua, matunda, michemiche ya matunda ili kuhakikisha matibabu yaliyo mazuri sana.

 

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post