" BARRICK YAPONGEZWA KWA KULIPA KODI VIZURI

BARRICK YAPONGEZWA KWA KULIPA KODI VIZURI

 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda akitoa ngao ya mlipa kodi nzuri kwa Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu Bw. Leon EbondoBarrick ni mlipa kodi nchni – TRA Na Mwandishi Wetu, Bulyanhulu Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imeipongeza kampuni ya uchimbaji wa madini nchini  Barrick ambayo inaendesha shughuli zake kwa ubia na serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga kwa kuchangia Pato la Taifa na kuwa na rekodi ya kulipa kodi vizuri na kufuata sheria za nchini.Pongezi hizo zimetolewa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda, baada ya kufanya ziara katika mgodi wa Barrick Bulyanhulu uliopo Halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja (Customer Service Week).Kamishna Mwenda ambaye aliongozana na ujumbe wa maofisa wa mamlaka hiyo alisema wameamua kuwatembelea Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa sababu unalimikiwa na kampuni kubwa na ni walipa kodi wazuri na wanafuata sheria na kanuni mbalimbali za nchini.“Migodi ya Barrick Bulyanhulu na Barrick North Mara ni wachimbaji wakubwa wa madini hapa nchini ni walipa kodi wakubwa na wazuri , tumewatembelea ili kujua changamoto zao katika shughuli za uchimbaji wa madini na kuangalia namna ya kuzitatua,” alisema Mwenda.Aliongeza migodi ya Barrick licha ya kuwa walipakodi wazuri pia imeajiri idadi kubwa ya wafanyakazi ambao wanalipa kodi sambamba na wakandarasi pamoja na wazabuni wanaofanya nao kazi na kuchangia katika ulipaji wa kodi ambapo wakijengewa mazingira mazuri watachimba madini zaidi na Serikali kukusanya zaidi kodi kutokana na uwekezaji wao.”Alifafanua kwamba mamlaka ya mapato ni mshirika (Partner) kwa walipa kodi wote hapa nchini hivyo wanatembelea walipa kodi ili kujua changamoto zao za kikodi kujifunza ni kodi zipi zinastahili na zipi hazistahili ili kufanyike maboresho kwa manufaa mapana ya pande zote.Pia ameipongeza kampuni hiyo kwa mchango mkubwa kwa jamii kupitia kanuni ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) ambapo jamii zinazozunguka migodi ya Barrick imekuwa ikinufaika na miradi kama vile maji, barabara, ujenzi wa mabweni ya shule , zanahati na miundombinu kwenye shule za sekondari na za msingi.Kwa upande wake Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu Bw. Leon Ebondo, amemshukuru Kamishna Mkuu wa TRA na Ujumbe wake kwa kufanya ziara mgodini hapo, na kuwasikiliza kwa lengo la kufanyia kazi na changamoto zao.Bw. Ebondo alisema Mgodi wa Barrick Bulyanhulu umeajiri wafanyakazi wengi wenye ajira za kudumu na wakandarasi wake mbalimbali ambapo pia wameajiri watanzania wengi kupitia zabuni mbalimbali zinazotoka kwenye migodi ya Barrick na wananchi wanaotoka katika vijiji vinavyozunguka mgodi wamekuwa wakipata ajira za muda.Mwaka jana katika wiki yam lipa kodi Mgodi wa dhahabu wa  Barrick North Mara ambao pia unamilikiwa kwa ubi ana serikali kupitia Twiga Minerals Corporation ilipata tuzo ya uzingatiaji kanuni za kodi nchini kitaifa na kwenye sekta ya madini katika kipindi cha mwaka wa 2023/24 katika hafla ya utoaji wa tuzo kwa walipa kodi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).Katika kipindi cha mwaka 2024, Twiga Minerals Corporation ililipa kodi ya mapato kiasi cha dola milioni 92,Mwaka 2023 ililipa dola milioni 58 na kipindi cha mwaka cha 2022 ililipa dola milioni 112Twiga ilichangia zaidi ya dola bilioni 4.24 katika uchumi wa Tanzania kuanzia kipindi cha mwaka 2019. Kati ya hizo, dola bilioni 1.37 zililipwa kwa njia ya kodi na tozo mbalimbali za serikali.Mwisho.Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda na Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu Bw. Leon Ebondo wakigonganisha glass mara baada ya kikao na majadiliano ya pamoja kwenye mgodi huo wa Bulyanhulu 


 

Post a Comment

Previous Post Next Post