" BURUTE SACCOS LTD YATIMIZA MSINGI WA SABA WA KUIJALI JAMII HASA KATIKA SHULE ZENYE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM KAGERA

BURUTE SACCOS LTD YATIMIZA MSINGI WA SABA WA KUIJALI JAMII HASA KATIKA SHULE ZENYE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM KAGERA

Na Lydia Lugakila, Misalaba Media BukobaChama cha ushirika cha akiba na mikopo kwa watumishi wa umma kwa wilaya za Bukoba na Missenyi Mkoani Kagera (BURUTE SACCOS LTD) kimetoa vitu mbalimbali yakiwemo madawati, vyenye thamani zaidi ya shilingi ilioni 40 katika shule za msingi zenye wanafunzi wa mahitaji maalum katika wilaya za Bukoba na Misenyi mkoani Kagera.Vitu hivyo vimegawiwa kwa wahitaji mnamo Oktoba 10,2025 na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe, Hajjat Fatma Mwassa ambaye amekuwa mgeni rasmi katika hafla fupi ya kugawa vitu hivyo iliyofanyika katika Ofisi za Manispaa ya Bukoba.Mwenyekiti wa Burute Saccos Charles Tegamaisho amevitaja vitu vilivyogawiwa kuwa ni pamoja na madawati 340, bima za afya kwa wanafunzi 47 shule ya mseto Tumaini, sukari kilo100, maharage kilo 200,  pampas box 6,  mashuka 240 na vyandarua 205."Saccos yetu inayo misingi saba ya ushirika na leo tumetimiza msingi wa saba wa kuijali jamii kwa kutoa vitu mbalimbali katika shule zenye watoto wa mahitaji maalum" amesema TegamaishoKwa upande wa mgeni rasmi katika tukio hilo ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe Hajjat Fatma Mwassa ameeleza kuwa, Saccos hiyo inafanya vizuri kuijali jamii hivyo akatoa wito kwa Saccos nyingine kufanya hivyo pale wanapopata ziada.Amesema wafanyabiashara wa kahawa na wale wenye viwanda vya kahawa mkoani Kagera na wenyewe kwa umoja wao wakusanye kitu na warudishe fadhira kwa wananchi."Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa wadau wote watakaojitokeza kuunga mkono juhudi za serikali katika kuchangia maendeleo ya wananchi hususan katika sekta ya elimu, afya na sekta nyinginezo" amesema Hajjat Mwassa.Aidha mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Bukoba Jacob Nkwera ameeleza kuwa, Manispaa hiyo ina shule za msingi za serikali zipatazo 26  ambazo zinahitaji miundo mbinu ya madawati 8,571 lakini hadi sasa kuna madawati 6, 373 na upungufu wa madawati 2,100.Amesema madawati yaliyotolewa na Burute Saccos yanakwenda kupunguza mapungufu yaliyopo katika shule hizo.Nkwera ameeleza kuwa, shule zilizopata madawati ni tano kila shule madawati 20, shule ya msingi Kashai ,Tumaini mseto, Mafumbo, Rwemishasha na Kashenge.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post