" UTPC ,IMS WAWANOA WAANDISHI WA HABARI KUANDIKA HABARI ZENYE TIJA

UTPC ,IMS WAWANOA WAANDISHI WA HABARI KUANDIKA HABARI ZENYE TIJA

Na Mwandishi wetu , IringaWaandishi wa habari nchini wametakiwa kuandika na kuzalisha maudhui yenye tija, ubora na viwango vinavyogusa maslahi ya umma na kuchochea maendeleo katika jamii badala ya habari nyepesi zisizo na mchango kwa jamii.Rai hiyo imetolewa na  mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation (TMF), Dkt. Dastan Kamanzi   leo mkoani Iringa wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) na IMS ,mafunzo yaliyoshirikisha waandishi wa habari na wadau wa habari ,mafunzo  yaliyolengwa  kuwajengea uwezo waandishi wa habari juu ya uandishi unaogusa uwajibikaji na kuchochea mabadiliko kwenye jamii.Dkt. Kamanzi alisema TMF inataka kuona uandishi wenye mguso na unaochochea uwajibikaji kwa viongozi na taasisi mbalimbali.“Tunataka uandishi unaogusa umma na maslahi ya jamii. Uandishi unapaswa kuwawajibisha watawala na kuwapa wananchi uelewa ili waweze kudai uwajibikaji. Ni uandishi unaojikita kuibua changamoto za kijamii na kusukuma utekelezaji wa majukumu kwa maslahi ya wote,” alisema.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC), Frank Leonard, aliwataka wanahabari kuachana na tabia ya kuwa "waandishi machawa" wanaoegemea upande mmoja na kusifia badala ya kuibua hoja muhimu za kijamii.“Kuna tatizo kubwa la kuibuka kwa aina mpya ya uandishi wa uchawa. Badala ya kufanya kazi ya kuibua changamoto, baadhi ya wanahabari wamekuwa wakijikita kwenye kusifia. Hatuendi sawa, lazima tubadilike,” alisema Leonard.Naye Victor Maleko kutoka Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), alisema mafunzo hayo yamelenga kuwaunganisha wanahabari na wananchi ili maudhui ya habari yazingatie maslahi ya jamii.“Semina hii imewapa waandishi nafasi ya kusikiliza changamoto za wananchi na kupata mawazo mapya yatakayosaidia kuboresha tasnia ya habari,” alisema.Akaongeza kuwa tafiti zinaonyesha kuwa kwa sasa sehemu ya jamii imepoteza imani na vyombo vya habari kutokana na kupungua kwa uandishi wa uchunguzi na habari zenye kuleta ufumbuzi wa changamoto.Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo walisema yamerudisha matumaini na hamasa katika tasnia ya habari.Mwandishi kutoka Shamba FM, Shani Nicolous, alisema mafunzo hayo yatawawezesha waandishi kuandika habari zenye majibu kwa jamii bila upendeleo.“Tumepoteza imani ya wananchi kutokana na kufanya kazi kwa hofu, lakini mafunzo haya yametupa dira. Tutakuwa daraja kati ya Serikali na wananchi kupitia habari zenye tija,” alisema.Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Iringa, Hakimu Mwafongo, alisema ni wajibu wa wanahabari kutenda haki kwa jamii wanayoihudumia.“Tuitendee haki jamii. Kalamu zetu zisaidie kuibua changamoto za wananchi na kuchochea maendeleo badala ya kufanya uandishi wa upendeleo,” alisema. Katika Mafunzo hayo yaliyoshirikisha pia wadau wa habari mwakilishi wa wadau hao  Raphael Mtitu, alisema matarajio yao ni kuona mabadiliko katika habari zinazoandikwa na wanahabari.“Tunataka waandishi wa habari waandike habari zinazogusa wananchi na kuleta mabadiliko. Huo ndiyo uzalendo wa kweli,” alisema Mtitu.Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation (TMF), Dkt. Dastan Kamanzi akitoa mafunzo.



 

Post a Comment

Previous Post Next Post