"
DKT. TULIA ACKSON AFIKA KATA YA ILEMI NA MWANSEKWA KUTOA HAMASA KWA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA KURA KWA AMANI IFIKAPO OKTOBA 29,2025
Na Lydia Lugakila, Misalaba Media Mbeya.Mgombea Ubunge wa Jimbo la Uyole kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 23 Oktoba 2025, amefanya ziara katika maeneo mbalimbali ya kata ya Ilemi na Mwansekwa, mkoani Mbeya.Katika ziara hiyo, Dkt. Tulia amewatembelea wananchi na wafanyabiashara wa kata ya Ilemi kwa lengo la kuwahamasisha kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.Pamoja na mambo mengine, Dkt. Tulia amewahimiza wananchi kushiriki uchaguzi kwa amani na utulivu, huku akiwahasa kuwachagua kwa kishindo wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia ngazi ya urais, ubunge hadi udiwani.
Post a Comment