Jeshi la Polisi nchini limetoa ufafanuzi kuhusu taarifa zinazosambaa mitandaoni zinazomhusu Ndugu Godbless Lema anmayedai kwamba usalama wa maisha yake upo hatarini.
Ufafanuzi huo unakuja kufuatia maombi kutoka kwa Waandishi wa Habari kuhusu suala hilo.
Msemaji wa Jeshi la Polisi kutoka Makao Makuu ya Polisi, Dodoma, amesema Jeshi hilo linaendelea kufuatilia kwa karibu taarifa hiyo.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi limemsisitiza Ndugu Lema afike katika Kituo cha Polisi ili aweze kuwasilisha taarifa yake hiyo rasmi na kwa njia zinazokubalika kisheria. Uwasilishaji wa taarifa rasmi utawezesha Jeshi la Polisi kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa taratibu za kisheria.
Aidha, Jeshi la Polisi limetoa wito na kusisitiza kwa baadhi ya viongozi wa wananchi kuendelea kuzingatia utaratibu wa kisheria wa kuwasilisha taarifa sahihi kwa mamlaka za Haki Jinai.
Lengo la wito huo ni kuepusha upotoshaji na taharuki zisizo za lazima ambazo huweza kusababishwa na taarifa zisizothibitishwa au kuwasilishwa katika maeneo yasiyo rasmi.
Taarifa hiyo iliyotolewa na Jeshi la Polisi imesisitiza umuhimu wa kufuata utaratibu na sheria wakati wote.
Post a Comment