"
KINJEKITILE: TUTABORESHA MIUNDOMBINU YA VIWANJA ILI KUKUZA VIPAJI
Na Osama Chobo, Misalaba Media - kilwa Mgombea ubunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini, kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Kinjekitile Ngombale Mwiru, ameahidi kuboresha miundombinu ya michezo endapo atapewa ridhaa ya kuwatumikia wananchi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.Akizungumza katika moja ya mkutano kampeni ulofanyika kijiji cha pungutini kata ya kinjumbi wilayani kilwa, Mhe. Mwiru alisema amejionea vipaji vingi vya vijana wa Kilwa Kaskazini katika michezo mbalimbali hususan soka, lakini changamoto kubwa ni ukosefu wa miundombinu bora ya viwanja na vifaa vya michezo.> “Nimetembelea kata kadhaa na kuona jinsi vijana wetu wanavyopambana, lakini viwanja vingi havina hadhi ya kuchezea. Tukipewa ridhaa, tutaboresha miundombinu hii ili vipaji viweze kuonekana na kutambulika kitaifa na kimataifa,” alisema Mhe. Mwiru.Ameongeza kuwa anafahamu michezo ni ajira halali kwa vijana wengi na imekuwa chanzo cha mafanikio kwa watu wengi duniani, hivyo ataweka mkazo katika kuboresha sekta hiyo ili iwe chachu ya maendeleo.> “Michezo ni ajira. Kuna mifano hai ya vijana waliojikwamua kutoka maisha magumu kupitia vipaji vyao. Nitahakikisha tunaanzisha mashindano ya ndani yatakayoratibiwa kwa utaratibu wa kisasa ili kuinua na kuonyesha vipaji vyao,” alisisitiza.Mhe. Mwiru pia amewataka wananchi wa Kilwa Kaskazini kuchagua Chama Cha Mapinduzi (CCM) ifikapo Oktoba 29, akisema ndicho chama pekee chenye dhamira ya kweli ya kuwaletea maendeleo endelevu katika nyanja zote ikiwemo michezo, elimu, afya na uchumi wa mtu mmoja mmoja.> “Tukishikamana na CCM, tutapiga hatua kubwa. Huu ni wakati wa kufanya maamuzi sahihi kwa ajili ya mustakabali wa vijana wetu na maendeleo ya Kilwa Kaskazini,” alisema kwa kuhitimisha.





Post a Comment