" NABII MPANJI AWATAKA WAUMINI NA WATANZANIA KWA UJUMLA KUJIEPUSHA NA MAANDAMANO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 29,2025

NABII MPANJI AWATAKA WAUMINI NA WATANZANIA KWA UJUMLA KUJIEPUSHA NA MAANDAMANO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 29,2025

Na Lydia Lugakila, Misalaba Media MbeyaMchungaji wa Kanisa la Gospel Miracle Church for All People (GMCL), Nabii David Mpanji, amewataka waumini wa kanisa hilo pamoja na Watanzania kwa ujumla, kujitenga na maandamano yoyote kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025 huku akisisitiza kuwa vitendo hivyo vinaweza kusababisha kupoteza amani, uchumi, na hata familia zao.Akizungumza Oktoba 26, 2025, katika ibada maalum iliyofanyika kanisani hapo jijini Mbeya, Nabii Mpanji amesema kuwa katika nchi nyingi, kuelekea kipindi cha uchaguzi mara nyingi huzuka vurugu na maandamano yasiyo na tija, ambayo huishia kuharibu mali, biashara, na maisha ya watu."Taifa hili ni zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, hivyo nawakumbusha Watanzania kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi niwaombe tarehe hiyo isiwe chanzo cha kupoteana na familia zenu,” alisema Nabii Mpanji.Aidha, ametoa wito kwa Watanzania kutojihusisha na watu wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii kushawishi maandamano au kuchochea vurugu ambapo amesisitiza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vipo tayari kuhakikisha amani inatawala.Amewashauri waumini hao baada ya kupiga kura,  warejee kanisani kuliombea Taifa na kuwa Viongozi wa dini wanalo jukumu kubwa la kulinda amani na kuhakikisha uchumi huo unabaki salama.Aidha nabii Mpanji amewataka viongozi wa dini kushirikiana na viongozi wa serikali katika kudumisha amani, akibainisha kuwa hakuna mtu anayefurahia kuona nchi ikiingia katika hali ya uharibifu."Ni wakati wa kushikamana ili kila ila mmoja awe mlinzi wa mwenzake, maana Tanzania ni ya kwetu sote,” alisema kwa kusisitiza.Hata hivyo amewahimiza Watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kuwachagua viongozi wao.



Post a Comment

Previous Post Next Post