" KURA YAKO NI SAUTI YA MAENDELEO: DKT. SAMIA ALIVYOBADILISHA TASWIRA YA MIUNDOMBINU TANZANIA

KURA YAKO NI SAUTI YA MAENDELEO: DKT. SAMIA ALIVYOBADILISHA TASWIRA YA MIUNDOMBINU TANZANIA

Dar es Salaam. Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, wananchi wanahimizwa kutumia haki yao ya kidemokrasia. 

Kauli ya "Kura yako ni sauti ya amani, daraja la maendeleo, na mwanga wa kesho bora" inawahimiza Watanzania "watoke" Oktoba hii, kwenda kupiga kura kama haki yao ya msingi.

Mfanyabiashara wa soko la Chifu Kingalu Morogoro Yusuf Hamad Brush anasema kwamba ni vyema watu wakatoka katika majengo yao na maeneo ya kazi kwenda kupiga kura Oktoba 29 kwa sababu hiyo ndio  maana ya maendeleo.

Anasema usipoenda kupiga kura utakuwa unajimnyima maendeleo yako mwenyewe na hasa uchaguzi wa mtu kukuwezesha kuwa na maendeleo unayoyataka.

Anasema uchaguzi ndio njia pekee ya kupanga maendeleo na Amani ya taifa.

Anasema yeye mwenyewe ataoenda kupiga kura kwa kuwa anaamini kwamba kura hiyo ndio msingi wa mabadiliko anayoyataka nchini.

Katika kuhimiza upigaji kura, rekodi ya mgombea Dkt. Samia Suluhu Hassan inatumiwa kama kielelezo cha maendeleo endelevu ya Taifa. Serikali yake imejikita katika kubadilisha taswira ya miundombinu nchini, jambo linalochukuliwa kama msingi wa kuendeleza uchumi na urahisi wa maisha.

Katika Sekta ya Usafiri na Miundombinu:

Utekelezaji wa miradi mikubwa unatajwa, ikiwemo kukamilisha ujenzi wa barabara ya juu ya Ubungo na kuanzisha mipango ya barabara za juu mikoani. Kazi kubwa inaendelea katika ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza, hatua muhimu itakayobadilisha usafiri nchini.

Dkt. Samia pia anatajwa kusimamia ujenzi wa madaraja makubwa kama Daraja la Kigongo–Busisi na Daraja la JPM, ambayo yanajenga daraja la maendeleo kwa kuunganisha mikoa kwa urahisi zaidi wa kibiashara na kijamii.

Aidha, juhudi zimefanywa kuboresha viwanja vya ndege vya kisasa katika mikoa muhimu kama Dodoma, Mwanza, na Kigoma, huku mfumo wa usafiri wa mwendokasi (DART) jijini Dar es Salaam ukiwa umeboreshwa kwa kuongeza njia mpya na magari ya kisasa.

Mbali na miundombinu ya usafiri, Dkt. Samia pia ametajwa kufanikisha ujenzi wa nyumba bora za watumishi wa umma kote nchini.

Wito unaendelea kutolewa kwa wapiga kura kutumia kura yao "kwa Samia" mnamo Oktoba, wakisisitiza kauli mbiu ya "Kazi na utu tunasonga mbele."

Post a Comment

Previous Post Next Post