Mgombea wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwasili mkoani Shinyanga kesho Jumamosi, Oktoba 11, 2025, kwa ajili ya kufanya mikutano ya kampeni.
Kwa mujibu wa ratiba ya ziara hiyo, Rais Samia ataianza kwa kuwasalimia na kuomba kura kwa wananchi wa Wilaya ya Kishapu kabla ya kufanya mkutano wa hadhara utakaofanyika kuanzia saa nne asubuhi katika Uwanja wa CCM Kambarage, mjini Shinyanga.
Baada ya mkutano huo, Dkt. Samia ataendelea na ziara yake mkoani humo ambapo anatarajiwa kufanya mkutano mwingine wa hadhara kuanzia saa nane mchana katika Uwanja wa Magufuli, Manispaa ya Kahama.
Akizungumza na Misalaba Media, Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Bwana Richard Raphael Masele, amethibitisha taarifa hizo na kuwakaribisha wananchi wote kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mikutano hiyo ya kampeni.
Masele amehimiza wananchi wa Shinyanga kutumia fursa hiyo kumsikiliza mgombea huyo wa CCM akieleza sera na ahadi zinazolenga kuleta maendeleo endelevu kwa Watanzania wote.
Post a Comment