HomeHABARI MGOMBEA AOMBA KUCHAGULIWA KWA KURA NYINGI Misalaba Media October 10, 2025 0 MGOMBEA wa nafasi ya udiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Nyamagana Mkoani Mwanza, Dkt. Frank Chacha ameendelea kunadi sera zake kwa wananchi kupata ridhaa ya kuchaguliwa kwenye uchaguzi utakaofanyika mwishoni mwa mwezi huu tarehe 29 Oktoba, huku akitaka wakaazi wa eneo hilo wajitokeze kwa wingi katika mchakato huo.Dk Frank Chacha aliwaomba wakazi wa mwanza wakichague chama cha mapinduzi kuanzia kiti cha urais,ubunge na madiwani ili kuchochea maendeleo ikiwemo kata ya nyamagana ambayo ni kitovu cha miradi ya kimkakati jijini hapa ili waweze kufikia ndoto kubwa za kiuchumi."Mkituchagua kwa utatu wetu tutaweza kuwaletea maendeleo katika eneo lenu" alisema Dk Chacha.Alitaja uwepo ujenzi wa hoteli ya Nyota tano inayojengwa na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kitovu cha kituo cha treni ya Mwendo Kasi (SGR), Mv mwanza sambaba na upanuzi wa bandari ya kisasa na miradi mingine kuwa itachochea shughuli za ukuaji wa kiuchumi kwa wakaazi wa eneo hilo.Dk Chacha aliwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi kuonesha mshikamano wao dhidi ya juhudi za maendeleo zilizooneshwa kufanywa na serikali ya awamu ya sita katika eneo hilo. 🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA You Might Like View all
Post a Comment