" MENEJA WA EWURA KANDA YA ZIWA KUJA NA MIKAKATI MIPYA YA KUTATUA CHANGAMOTO KWA WATEJA

MENEJA WA EWURA KANDA YA ZIWA KUJA NA MIKAKATI MIPYA YA KUTATUA CHANGAMOTO KWA WATEJA

Na Mwandishi wetu, Misalaba Media

Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Ziwa, George Mhina amewataka wananchi kufahamu na kuzingatia mikataba inayoelekeza kutekelezwa baina ya watoa huduma na wateja.

Ameyasema hayo Leo Jijini Mwanza ambapo ameeleza kuwa upo umuhimu mkubwa wa kufahamu mikataba iliyopo kati ya watoa huduma za maji na wananchi kwani hali hiyo huwawezesha wateja kulinda haki zao kuvunjwa na hivyo kuleta usumbufu kwa wananchi.

"Ni wajibu kwa taasisi kutekeleza majukumu yao vizuri hivyo tunaamini wiki hii imekuwa ni faraja kwa wananchi kwani wamefika zaidi ya 200 kupata elimu na kuuliza maswali " alisema Mhina.

Alisema kwa sasa wameanza utoaji wa huduma kidijitali ili kupunguza usumbufu kwa wateja kufuatilia huduma mbalimbali ikiwemo leseni hata bila ya kufika ofisini kwao.

Post a Comment

Previous Post Next Post