Na Elisha Petro, Misalaba Media
Mgombea udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Ndala Bi. Zamda Shabani Mwebea amehitimisha rasmi kampeni zake za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Jumatano, Oktoba 29, 2025.
Katika kuhitimisha kampeni hizo Bi. Zamda amefanya ziara katika mitaa yote mitano ya kata ya Ndala ikiwemo Ndala, Mlepa, Mwabundu, Mapindu, na Banduka ambapo amewashukuru wananchi kwa ushirikiano waliompatia kipindi chote cha kampeni na kuwasihi wajitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura.
Akizungumza mbele ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza Bi. Zamda amewahakikishia wakazi wa Ndala kuwa endapo watampa ridhaa ya kuwa diwani atajikita katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili kata hiyo ikiwemo Kuboresha miundombinu ya barabara,kuimarisha huduma za afya na elimu na kusukuma mbele ajenda za maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
“Nawaomba wananchi wenzangu wa Ndala, tujitokeze kwa wingi Oktoba 29. Tupige kura ya amani, kura ya maendeleo, kura ya ushindi. Mimi Zamda Mwebea, nina dhamira ya kweli ya kuwatumikia,” amesema Bi. Zamda
Aidha, Bi. Zamda pia amewahimiza vijana kutojihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani na kujiepusha na maandamano bali wajiandae na kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura pamoja na kuwa mabalozi wa utulivu na mshikamano kabla, wakati na baada ya uchaguzi.
“Vijana ni nguvu ya taifa msiruhusu mtu yeyote awatumie kuvuruga amani tuliyoijenga kwa miaka mingi wala msitumike kuandamana kwani maandamano yanarudisha nyuma maendeleo badala yake tumieni nguvu zenu kuhakikisha mnafika vituoni kupiga kura"
Akihitimisha hotuba yake Bi. Zamda amewahakikishia wananchi kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitaendelea kuwa nguzo ya maendeleo nchini, kikitekeleza kwa vitendo ahadi zake za kuwaletea Watanzania maisha bora zaidi.
“CCM ni chama cha watu, chama cha maendeleo tutaendelea kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi kwa kasi na ufanisi mkubwa,”
Kampeni hizo zilianza August 28,2025 na zinatarajiwa kuhiyimishwa kitaifa October 28,2025.
Mgombea udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Ndala Bi. Zamda Shabani Mwebea akizungumza.
Post a Comment