Mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi (CCM)
Taifa, Gasper Kileo 'Gaki', ametembelea ujenzi wa Daraja la Kasenga
linalounganisha Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga na Wilaya ya Kaliua mkoa
wa Tabora.
Daraja hilo ni miongoni mwa madaraja manne yanayojengwa katika Halmashauri ya
Ushetu, likiwa na urefu wa mita 80 na thamani ya shilingi bilioni 5.
Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo, MNEC Gaki amesema
ameridhishwa na kasi ya ujenzi na ubora wa kazi inayoendelea.
Ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia
Suluhu Hassan kwa kuona na kutatua kero ya wananchi iliyodumu kwa muda mrefu.
“Mradi huu ni ushahidi wa dhahiri wa jinsi Serikali ya CCM inavyosikiliza na
kutatua changamoto za wananchi. Kupitia daraja hili, uchumi wa Ushetu
utaimarika kwa kuwa sasa linaunganisha mikoa miwili na kurahisisha shughuli za
kijamii na kiuchumi,” alisema Gaki.
MNEC Gaki ametembelea eneo hilo leo akiwa njiani kuelekea kwenye mkutano wa
kufunga kampeni za Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ushetu kupitia CCM, Ndg. Emmanuel
Cherehani, unaofanyika katika kijiji cha Bugomba B, kata ya Ubagwe.





Post a Comment