Mgombea wa nafasi ya udiwani wa Kata ya Kolandoto kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw. Moses Mshagatila, ameahidi kushirikiana kwa karibu na uongozi wa Shule ya Msingi Mwamagunguli, kijiji cha Mwamagunguli na kata nzima ya Kolandoto katika shughuli zote zinazochochea maendeleo.Bw. Mshagatila ametoa ahadi hiyo wakati akiwahutubia wazazi, wanafunzi na wananchi katika mahafali ya darasa la saba ya Shule ya Msingi Mwamagunguli A ambapo ameahidi kuwa ataratibu zoezi la ujenzi wa choo cha walimu chenye matundu mawili katika shule hiyo ili kuboresha utendaji wao wa kazi.Katika hatua nyingine, Bw. Moses Mshagatila ameuahidi uongozi wa shule, wananchi wa kijiji cha Mwamagunguli na Kata ya Kolandoto kuwa endapo atapata ridhaa ya kuwa Diwani wa Kata ya Kolandoto ataendelea kushirikiana nao bega kwa bega katika kutekeleza miradi ya kijamii ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya shule, barabara na huduma za kijamii.“Mimi nawaahidi ushirikiano wa dhati, nawaahidi kuwa pamoja nanyi katika kila shughuli za maendeleo ya shule yetu, kijiji chetu na kata nzima ya Kolandoto na naahidi kuwa kila mwanafunzi atakayefaulu nitamnunulia Counter book tano ili akaanze nazo masomo ya sekondari na ninayo kauli mbiu yangu inayosema KOLANDOTO YETU KESHO YETU, KESHO YETU KOLANDOTO YETU - amesema Bw. Mshagatila Aidha, amemalizia kwa kuwataka wazazi na walezi kuendelea kushirikiana na walimu katika malezi na elimu ya watoto akisisitiza kuwa mafanikio ya wanafunzi ni matokeo ya ushirikiano wa wadau wote wa elimu.Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Adam Mbega amewataka wazazi kuwajibikia vyema jukumju la makuzi na malezi ya watoto ili waweze kutimiza ndoto zao. " jukumu la malezi halipaswi kuachiwa walimu pekee yetu bali wazazi mnanafasi kubwa sana ya kuwalea hawa watoto wanapokuwa huko majumbani, tunapaswa kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha watoto wanalelewa katika maadili mema na nidhimu bora naomba tuwatunze hawa watoto muwatunze,” amesema mwalimu Mbega. Wakati huohuo, wazazi wamewashukuru walimu kwa moyo wao wa mjitoleo kuwafundisha watoto wao toka chekechea hadi kuhitimu Elimu ya msingi na wakiahidi kuendelea kushirikiana nao kwa mambo yote ili kuhakikisha shule hiyo unaendelea kufanya vizuri kitaaluma."Sisi wazazi tunawashukuru sana walimu kwa kazi kubwa mliyoifanya kwa hawa watoto wetu wanaohitimi leo mmefanya kazi kubwa sana na msichoke tuunganiahe nguvu kuwasaidia hata hawa wanaobaki hakika umoja utaifanya shule yetu iwe kufanya vizuri kitaaluma ndani ya Mkoa na kitaifa pia"Jumla ya wahitimu 27 wamefanikiwa kuhitimu Elimu ya msingi katika shule hiyo kwa mwaka 2025 ambapo wameahidi kuendelea kusoma kwa kadri wanavyopata nafasi ya kuendelea na Elimu ya sekondari.
Mgombea wa nafasi ya udiwani wa Kata ya Kolandoto kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw. Moses Mshagatila, akizungumza kwenye mahafali hayo.
Mgombea wa nafasi ya udiwani wa Kata ya Kolandoto kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw. Moses Mshagatila, akizungumza kwenye mahafali hayo. 
















Post a Comment