"
MWIRU: TUTATAFUTA BOTI ZA KISASA ZENYE GHARAMA NAFUU KWA WAKAZI WA KILWA KASKAZINI
Na Osama Mohamedi chobo, Misalaba Media -kilwa Mgombea ubunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Kinjekitile Mwiru, ameendelea na kampeni zake za kunadi sera kwa wananchi wa Kata ya Somanga, ambapo ameahidi kuhakikisha anatafuta boti za kisasa zenye gharama nafuu ili kuwawezesha wavuvi na wakazi wa maeneo ya pwani kujikwamua kiuchumi.Akizungumza na wananchi wa kata hiyo, Mhe. Mwiru amesema kuwa moja ya changamoto kubwa kwa wakazi wa eneo hilo ni ukosefu wa vyombo vya usafiri wa baharini vinavyokidhi mahitaji ya wananchi wa kipato cha chini.> “Mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi na mkanipa ridhaa ya kuwa mbunge wenu, nitahakikisha tunatafuta boti za gharama nafuu ambazo zinaendana na hali ya kipato cha wananchi wetu. Lengo ni kuwawezesha wavuvi wetu kufanya kazi zao kwa ufanisi na kuongeza kipato,” alisema Mhe. Mwiru.Aidha, aligusia kuhusu boti zilizotolewa kupitia mpango wa serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, akisema kuwa nazo zitasaidia kwa kiasi kikubwa, lakini bado kuna haja ya kuongeza juhudi ili wananchi wengi zaidi wanufaike.> “Boti za Mama Samia zipo, na tunazishukuru sana. Hizi zitasaidia kuongeza nguvu katika ajira, lakini bado tutatafuta boti nyingine zaidi ili kuwafikia watu wengi zaidi,” aliongeza.Katika hatua nyingine, Mhe. Mwiru aliwahamasisha vijana kuunda vikundi ili waweze kunufaika na mpango huo, akisema kuwa serikali itakuwa tayari kusaidia vikundi vya vijana watakaokuwa tayari kujituma na kutumia fursa hizo.> “Vijana wa Somanga na maeneo mengine ya Kilwa Kaskazini mtumie fursa hizi. Undeni vikundi, muwe tayari kufanya kazi, sisi tutasimama nanyi kuhakikisha mnapata boti na vifaa vya kazi ili muondokane na changamoto ya ajira,” alisisitiza.Mhe. Mwiru aliwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura na kufanya maamuzi sahihi kwa kumchagua kiongozi mwenye dira ya maendeleo






Post a Comment