" OKTOBA 29: TUJITOKEZE KWA WINGI KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA – KURA KWA CCM

OKTOBA 29: TUJITOKEZE KWA WINGI KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA – KURA KWA CCM

Na: Dkt. Reubeni Lumbagala, Misalaba Media -TangaKwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Uchaguzi Mkuu hufanyika kila baada ya miaka mitano. Kwa kuwa Uchaguzi Mkuu wa mara ya mwisho ulifanyika mwaka 2020, basi mwaka huu wa 2025, tunafanya Uchaguzi Mkuu. Uchaguzi Mkuu ni fursa adhimu ambapo wananchi wanapata nafasi ya kuchagua viongozi watakaowaongoza katika kipindi cha miaka mitano ijayo yaani 2025-2030.Kutokana na upekee wa tukio hili, kwa sasa siku ya Uchaguzi Mkuu ni siku ya mapumziko ya kitaifa ambapo wananchi wanapata fursa ya kwenda katika vituo walivyojiandikisha ili kupiga kura kwa uhuru ili kuchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani.Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kujinadi katika mikoa mbalimbali hapa nchini kuomba ridhaa ya kuongoza wananchi. Aidha, katika mikutano hiyo, Dkt. Samia anawaombea kura pia wagombea Ubunge na Udiwani watokanao na CCM ili kukamilisha "Mafiga Matatu" ambapo wakifanya kazi kwa pamoja huku wakiongoza na Ilani ya CCM ya mwaka 2025-2030, mambo yatakuwa mazuri zaidi.Siku ya Jumatano ya Oktoba 29, 2025, ni "Samia Day." Katika siku hii, wananchi wanashauriwa kupiga kura kwa wingi kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan katika nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani watokanao na CCM kama sehemu ya kutambua kazi kubwa na nzuri zilizofanyika katika kuharakisha maendeleo.Kazi nzuri zenye kugusa maisha ya wananchi katika sekta za elimu, maji, afya, miundombinu, kilimo, uvuvi, madini, ufugaji, biashara, umeme, ajira, uwekezaji kutaja kwa uchache zimefanyika na hivyo kuchangia katika kukuza maendeleo nchini.Dkt. Samia amefanya kazi kubwa katika kuongeza ukusanyaji wa mapato, hali inayochochea utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo inahitaji raslimalifedha kwa kiwango kikubwa katika utekelezaji na ukamilishaji wake.Upo umuhimu mkubwa sasa kwa wananchi kupiga kura kwa Dkt. Samia na wagombea wengine wa CCM kama msingi wa kuhakikisha ushindi wa kishindo unapatikana. Oktoba 29, 2025, jambo ni moja tu: Tunatiki, Tunatiki, Tunatiki. Tunatiki kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wagombea Ubunge na Udiwani watokanao na CCM.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post